Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe kumsimamisha kazi mtumishi George Mboje na kumuondoa kwenye timu ya Operesheni Korosho.

Pamoja na kumundoa kwenye timu hiyo pia Katibu Mkuu ametakiwa kumuondoa kwenye Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko."Katibu Mkuu, nataka umuondoe huyu George kwenye hii timu na pia sitaki kumuona kwenye Bodi na Taasisi yoyote katika Wizara ya Kilimo" Alisisitiza Mhe Hasunga .

Mhe Hasunga ametoa agizo hilo leo tarehe 4 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Watendaji wa timu ya Oparesheni korosho kilichofanyika katika ukumbi wa CBT Mkoani Lindi na wakati wa kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018.

George Mboja ambaye yupo kwenye timu ya Oparesheni Korosho akiwakilisha Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko anatuhumiwa kwa Utovu wa nidhamu sambamba na kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo wakati wa Oparesheni Korosho inayoendelea nchini.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018 mkoani humo. (Picha Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo).
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018 mkoani humo.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mhe Sarah Chiwamba, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe Christopher Ngubiagai wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018 mkoani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...