Mwandishi Wetu, MARA.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza kutokuandikishwa mpaka wazazi wao walipe michango wanaodaiwa katika shule mbalimbali jimboni kwake Mwibara, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara.  Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, amemtaka Afisa Elimu wa Kata ya Chitengule, Jimboni humo, Thadeo Lukinisha kuruhusu shule za msingi zilizopo katika Kata yake kuandikisha wanafunzi hao bila kikwazo chochote kwakuwa elimu ya shule ya msingi ni bure nchi nzima.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Nakatuba katika Kata hiyo, Lugola alipiga marufuku utaratibu huo ambao amesema hauna msingi wowote kwasababu unawaonea watoto ambao hawana kosa lolote hata kama kuna madeni ambayo wazazi wa wanafunzi hao wanadaiwa kutokana na watoto wao wanaoendelea na masomo katika shule zilizopo jimboni humo. 

 “Huu utaratibu sio sawa, haukubaliki, kipindi hiki wanafunzi wanaandikishwa kuanza darasa la kwanza waandikishwe bila kikwazo chochote ili waweze kupata elimu yao kama inavyostahili, michango yenu haihusiani na wanafunzi kuanza shule,” alisema Lugola. 

Hata hivyo, Afisa Elimu huyo tukio hilo lipo lakini walifanya hivyo kutokana na baadhi ya wazazi kutolipa kiasi cha shilingi mia nne ambayo inachangwa kwa ajili ya kila mwanafunzi anachangia kwa ajili ya kumlipa mpishi pamoja na mafuta ambayo fedha hiyo inalipwa kwa mwaka. Lugola alipata taarifa hiyo ya wazazi kukataliwa kuandikishwa watoto wao kuanza darasa la kwanza, baada ya mzazi mmoja kuulalamikia utaratibu huo na kuwafanya wazazi kutokuanidisha watoto hao kutokana na kudaiwa michango hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimsalimia Mkazi wa Kijiji cha Namalebe, Kata ya Chitengule, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, Kaswanila Molore kabla ya kuanza mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kijiji hicho. Akizingumza na wananchi wa Kata hiyo, Lugola amepiga marufuku wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza kutokuandikishwa mpaka wazazi wao walipe michango wanaodaiwa katika shule mbalimbali jimboni humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...