Na Felix Mwagara, (MOHA), MARA.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema wapo baadhi ya watu ambao wanajipenyeza kupitia mgongo wa taasisi za dini nchini kujifanya wahubiri kumbe ni wachochezi na wanajiingiza katika masuala ya kisiasa.

Amesema Wizara yake ipo makini katika kusajili Makanisa na Misikiti yote nchini na mpaka sasa wana maombi mengi ambayo yametumwa wakiomba kusajiliwa ambapo baadhi yao bado hayajasajiliwa kwasasababu wanahitaji umakini mkubwa katika kufanya uchunguzi wa kina kabla hawajatoa usajili ikiwa na lengo la kuepusha baadhi ya taasisi za dini zenye mpango mbaya na maendeleo ya  nchi.  

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Sunsi, Kata ya Nampindi, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, jana, Lugola ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo, alisema taasisi za dini zina mchango mkubwa nchini na uwepo wao ni muhimu katika maendeleo ya nchi, na serikali inawathamini mchango wao katika kuimarisha amani na pia kuwaweka watu pamoja lakini kuna baadhi ya dini hizo zinakiuka utaratibu wa usajili na kuvunja sheria za nchi kwa kuacha kuhubiri masuala ya kiroho wanajihusisha na masuala ya kisiasa pamoja na uchochezi. 

“Serikali ya Rais Dk. John Magufuli ya Awamu ya Tano haitakua tayari kwa mwananchi yeyote kutumia mwavuli wa dini, au kufanya misikiti na makanisa kuwa kichaka kwa kufanya uchochezi katika nchi hii, kuhatarisha amani ya nchi hii, tupo makini na hatuwezi kuchezewa na mtu yeyote au taasisi yoyote,” alisema Lugola.
 AZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Kata ya Nampindi, Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Sunsi Wilayani humo leo. Katika hotuba yake, alitoa onyo kwa baadhi ya watu wanajipenyeza kupitia mgongo wa taasisi za dini kujifanya wahubiri kumbe ni wachochezi na wanajiingiza katika masuala ya kisiasa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akicheza na Wanakwaya wa Kijiji cha Busambu, Kata ya Nampindi, jimboni kwake Mwibara, Bunda kabla ya kuanza mkutano wake wa kwanza kati ya minne na wananchi wa Kata hiyo, mkoani Mara. Lugola aliwataka wananchi wa Kijiji hicho kufanya maandalizi ya kilimo ili wasije kukumbwa na njaa kwa hapo baadaye endapo hawatalima. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...