Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameliagiza Shirikisho la vyama vya ushirika Tanzania (TFC) kushirikiana vyema na Chama Kikuu cha Ushirika Njombe (NJORECU) kuhakikisha kuwa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha Mbolea unaanza mapema kabla ya mwezi June mwaka 2019.

Alisema kuwa ujenzi wa kiwanda cha Mbolea utakapokamilika utawanufaisha wanaushirika wa chama hicho cha NJORECU sambamba na wakulima wote nchini kwani kitaongeza urahisi wa upatikanaji wa mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu kwa kuzalishwa hapa nchni.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 11 Disemba 2018 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Njombe, Mjumbe kutoka Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) pamoja na muungano wa makampuni ya uwekezaji kutoka China.

Mhe Hasunga aliwashauri kuandaa andiko la mradi huo litakaloeleza aina ya mbolea itakayozalishwa na taarifa zote zinazohitajika katika kufanikisha mradi huo kuanza.Wawekezaji hao kutoka nchini China kwa kushirikiana na chama kikuu cha Ushirika Njombe (NJORECU) wanataka kuwekeza katika ujenzi wa Kiwanda cha mbolea na kiwanda cha kufungasha Viuatilifu vinavyotumika katika mazao ya Kilimo.

Katika kikao hicho walieleza kuwa wawekezaji hao wapo tayari kuchangia asilimia 40% na NJORECU (kwa maana ya Tanzania) asilimia 60% katika ukamilifu wa ujenzi wa kiwanda hicho.Kutokana na umuhimu na uhitaji wa Mbolea nchini mjumbe wa bodi ya NJORECU alimweleza Mhe Waziri wa Kilimo kuwa wamekwishapeleka maombi ya kuomba kushirikiana na NSSF katika uwekezaji huo na wanasubiri majibu. 

Wakati huo hu, Waziri wa Kilimo Mhe Hasunga amekutana na kufanya mazungumzo na watendaji wakuu wa kampuni mbalimbali zinazojihusisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ndani na nje ya nchi-Business Network International (BNI).

engo la mkutano huo ilikuwa ni watendaji wakuu hao kujitambulisha na kumueleza Waziri wa kilimo shughuli wanazozifanya ili kuongeza ufanisi katika ushirikiano na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.BNI ni muungano wa makampuni 8 yanayowahusisha wafanyabiashara kati ya 30 Duniani.
Waziri wa Kilimo Mhe Hasunga (Mb) Mwenye Tai, akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa kampuni mbalimbali zinazojihusisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ndani na nje ya nchi-Business Network International (BNI) mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na watendaji hao Jijini Dar es salaam, leo tarehe 11 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Njombe, Mjumbe kutoka Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) pamoja na muungano wa makampuni ya uwekezaji kutoka China, leo tarehe 11 Disemba 2018 Jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...