Dixon Busagaga, Rombo.

MTU mmoja aliyefahamika kwa majina ya Colman Massawe mkazi wa Rombo amenusurika kufa alipofanya jaribio la kujiua kwa kukata shingo yake kwa kutumia Wembe muda mfupi baada ya kuhukumiwa kwenda jela miezi minne.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Massawe alihukumiwa kwenda jela miezi minne baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya kuvunja nyumba usiku na kuiba .

“Jana (Juzi)  ilikuwa ni siku ya hukumu yake na alihukumiwa kwenda jela miezi minne, lakini cha ajabu  ni kwamba kijana huyo ambaye alitokea gerezani wakati wa kufikishwa mahakamani hapo, aliingiza mkono mfukoni na kutoa kiwembe kipya na kuanza kujichinja” alisema Kamanda Issah.

Kamanda Issah alisema tukio hilo lilitokea muda mfupi wakati askari wakimpeleka kwenye gari, tayari kupelekwa gerezani ndipo alipochukua uamuzi huo wa kujikata sehemu koromeo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...