NA DENIS MLOWE, IRINGA

CHAMA cha Mapinduzi mkoa wa Iringa, kimemchagua mwadhili wa chuo kikuu cha Ruaha mkoani hapa, Dk. Abel Nyamahanga kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho kuchukua nafasi ya mwenyekiti aliyejiuzulu ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila.

Wajumbe 597 kati ya 631 waliohudhuria wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti mpya wa chama hicho chini ya msimamizi wa uchaguzi aliyekuwa waziri mkuu awamu ya nne, Mizengo Pinda.

Mkutano huo maalum uliohudhuriwa na wadau mbalimbali mkoani hapa ulikuwa wa upinzani mkali ambapo kutokana na wajumbe waliozidi akidi ya matakwa ya mkutano wa CCM mkoa kwa mujibu wa maelekezo ya kanuni za uchaguzi wa CCM wajumbe wote ni 631.

Wajumbe hao walitakiwa kuwapigia kura wanachama watatu ambao ni Vitusi Mushi, Amani Mwamwindi na Dk. Abel Nyamahanga ambao majina yao yalirudishwa kutoka kamati kuu ya CCM taifa kwa lengo la kupigiwa kura. Katika uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kichangani, wajumbe walilazimika kurudia uchaguzi kwa awamu ya pili baada ya awamu ya kwanza mshindi kutovuka nusu ya kura zilizopigwa kutokana na upinzani mkali.

Baada ya matokeo kutoka ndipo wa majina mawili ya Amani Mwamwindi na Dk. Abel Nyamahanga yalipigiwa kura kutokana na wajumbe 548 waliobaki baada yaw engine kutoka ukumbini na kuweza kupata mwenyekiti mpya baada ya Vitus Mushi kupata kura chache zaidi ambazo hazikukidhi kanuni za uchaguzi wa CCM. 
Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Iringa Dk Abel Nyamahanga akiwa na wagombea wa nafasi hiyo. kushoto kwake ni Aman Mwamwindi na kulia kwake ni Vitus Mushi.

 Baadhi ya wajumbe wa mkutano maalum wa uchaguzi wa mwenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa wakiwa ukumbini kabla ya zoezi la kupiga kura
 Msimamizi wa uchaguzi wa mwenyekit wa ccm mkoa wa Iringa Mizengo Pinda akizungumza kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza katika uchaguzi wa Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Iringa uliofanyika katika ukumbi wa Kichangani.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...