Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally amepokelewa Mkoa wa Mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera

Ndugu Bashiru anafanya ziara ya siku mbili kuimarisha Chama Mkoani Mara ikiwa na pamoja na kutembelea Wilaya ya Butiama alikozikwa mwasisi wetu Mwl. Julius kambarage Nyerere (Baba wa Taifa) Wilaya ya Bunda,Wilaya Musoma Mjini pamoja na Tarime.

Aidha, Ndg. Bashiru Ally amesema katika ziara yake hii ni kukijenga chama na kukiimarisha katika Misingi iliyowekwa na Mwasisi wetu Mwl.Nyerere. Ameyasema hayo Mbele ya wananchi aliapoanzia ziara yake Wilaya ya Bunda na baadaye kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa Utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi Mkuu wa CCM 2015/2020 wakiwa wanakagua kituo cha Afya jimbo la Bunda.

Ndugu Bashiru Ally, Baada ya Wilayani Bunda alielekea Wilayani Butiama kwa Mapokezi Makubwa ya asili ya Nyimbo za Kizanaki (LITUNGU na ZEZE) Huku wakiimba na kucheza na Baada ya Mapokezi hayo katibu Mkuu aliweka shada la Maua katika Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwl J.Kambarage Nyerere akiwa ameongozana na Viongozi Mbali mbali wa Chama na Serikali.

Akitoa neno la Shukrani Balozi wa China Nchini Tanzania baada ya kuweka Shada la Maua ktk Kaburi la Mwalimu amesema Baba wa Taifa hayati Mwl Nyerere watu wa China tutaendelea kumkumbuka Daima ktk maisha yetu hasa alipowasili nchini China Mwaka 1964

Dkt.Bashiru Ally ametoa salamu za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Ndugu John Pombe Joseph Magufuli kwa wana Mara na kuwambia anawahakikishia kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Mkoa na Uwanja wa ndege wa kisasa Musoma itatekelezwa.

Katibu Mkuu aliongozana na Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Canal Lubinga,Mwenyekiti wa CCM Mkoani Mara ndugu Samweli Niboye(Namba tatu) Mjumbe wa baraza la wadhamini CHAMA Taifa ndugu Gachuma pamoja na Viongozi wa serikali ngazi ya Mkoa na Wilaya.

Katibu Mkuu wa CCM amehitimisha kikao hicho kwa kusisitiza Umoja kwa watumishi wa Chama na Serikali, kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaendeleza misingi iliyo asisiwa na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Huu ni Mwendelezo Wa Uimarishaji wa Chama Cha Mapinduzi kanda ya ziwa

Imetolewa na:

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI 
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally akizungumza jambo mara baada ya kupokelewa na baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali alipowasili alikozikwa mwasisi wetu Mwl. Julius kambarage Nyerere,Butiama mkoani Mara .
Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally pamoja na Balozi wa China Nchini Tanzania wakiweka shada la Maua katika Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwl J.Kambarage Nyerere,huku Viongozi Mbali mbali wa Chama na Serikali wakishuhudia tukio hilo.
Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally akiwa ameongozana na baadhi ya viongozi wa chama wakikagua kituo cha Afya jimbo la Bunda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...