Na. Vero Ignatus, Arusha


Waumini wa dini ya Kikristo Jijini Arusha wametakiwa kulipa kodi ya serikali kama inavyotakiwa siyo kuiba, kwani wao wanatakiwa kuwa mfano bora wa kuigwa katika jamii inayowazunguka

Hayo yamesemwa na Makamu wa Askofu Dayosisi ya kaskazini Kati Gidion Kivuyo alipokuwa akihubiri katika katika la KKKT Usharika wa Engarenarok uliopo Jiji Arusha.

Amesisitiza kuwa kumjua Mungu Pamoja na kukataa rushwa, kutokuiba mali ya serikali kwani hata neno la Mungu linasisitiza kulipa kodi.'' Lipeni kodi ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu nanukuu maandiko siyo mimi''Alisema Mchungaji Kivuyo.Amewataka waumini hao kuishi maisha safi ya kuigwa maana ni chachu katikati ya kwa watu wengine wanaowatazama ambapo uadilifu, nidhamu na uchaji ambao kizazi kijacho kitajifunza kutoka kwao.

Amewasisitiza kuwa na utayari na kujifunza,akisema uanafunzi ni pamoja na kujikana wenyewe, kuepuke mambo ambayo siyo sahihi katika imani yao, na waenende sambamba na neno la Mungu linavyowataka.

Amewataka kujifunza na kutafakari siyo kufuata mkumbo bila Kuwa na mipangilio katika maisha bila kusahau uzalendo na kuchunguza mambo kwa kina.
'' Kuna watu wanaojifunza bila kufuzu mafunzo ya kweli, msiwe watu wasiopenda mema na kupenda anasa bali dumuni katika kweli ya Mungu ambayo itawaweka huru,epukeni kutangishwatangishwa kwenye mafundisho ya uongo nakupenda fedha" Alisema.

Amewataka kuwa na uelewa kwamba Imani haijengwi juu juu bali kwa mafundisho, huku akiwataka kuepuka utumwa ambao utawafanya mateka.
Amewaonya waumini hao na kuwataka makini na mafundisho ya uongo ambayo yanayogusa hisia lakini hayafundishi ukweli bali ni misisimko na wala hayana ukweli sawasawa na Mungu anavyoamuru.

Kadhalika amewasisitiza kufanya kazi kwa bidii iliwaweze kupata mafanikio sambamba na kulipa kodi ya serikali, na siyo kuzurura hovyo. '' Wacheni kuzunguka kwenye maombi kila mahali unachelewa wenzio wamefungua biashara zao na wamefanikiwa, wewe kutokana na kutokutulia kwako unabakia ukilaumu'' alisema

Amewaataka viongozi wa kanisa hilo kuwakumbusha waumini wao neno la Mungu mara kwa mara na kuwafundisha, Kutambua, kujuta, kutubia, kupokea, kuishi maisha na dhamiri safi mbele za Mungu. Amewataka kuweka malengo ya mwaka 2019 na siyo kuishi bila utaratibu ili waweze kurejea katika msingi mzuri wa kanisa hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...