Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

MKEMIA Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dk. John Magufuli, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanya chunguzi mbalimbali na kuwa miongoni mwa maabara bora za uchunguzi kwa nchi za Afrika Mashariki.

Dk.Mafumiko ameyasema hayo jijini Da es Salaam wakati anazungumza na maofisa uhusiano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo pamoja na waandishi wa habari katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya inayoendeshwa chini ya uratibu wa Wizara ya Afya.

Dk. Mafumiko amesema kuwa taasisi hiyo imeongeza uwezo zaidi wa kufanya uchunguzi wa kimaabara kwa kuchukua muda mfupi kutokana na serikali kununua mitambo ya kisasa ya uchunguzi inayowezesha kufanya uchunguzi kwa muda mfupi na kutoa majibu kwa haraka ukilinganisha na miaka mitatu iliyopita.

Amesema katika utoaji huduma za uchunguzi kwa muda mfupi na kusaidia vyombo vingine vya Serikali katika utoaji wa haki.

" Katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais, Dk. John Magufuli tumefanikiwa kuongeza mitambo mikubwa mitano ya kisasa ambayo imesaidia kuongeza ufanisi katika uchunguzi wa kimaabara na kutoa majibu kwa muda mfupi. Mtambo kama LCMS/MS unaweza kutoa majibu ya uchunguzi ya dawa za kulevya ndani ya saa moja kitu ambacho miaka mitatu nyumba ilikuwa ni ngumu ambapo ilihitajika mpaka siku saba kuweza kukamilisha uchunguzi wa namna hiyo," Dk.Mafumiko.


Pia amesema katika uchunguzi waliofanya ni pamoja ya kupambana na dawa za kulevya ambapo ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na vyombo kama Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya na Jeshi la Polisi kwa pamoja zimesaidia kupunguza matumizi ya dawa za kulevya kwa kuweka udhibiti imara wa kuingia nchini pia ufuatiliaji kwa watumiaji wa ndani ya nchi.

Aidha amesema kati ya matokeo makubwa katika miaka mitatu ni pamoja na kushiriki katika masuala makubwa ya kitaifa kama kuanguka kwa majengo, kuzama kwa meli Mv. Nyerere, ajali ya moto iliyotokea Musoma kwa kuwezesha kufanya uchunguzi uliowezesha baadhi ya marehemu kutambulika kupitia uchunguzi wa vinasaba na matukio mengine mengi ya kitaifa ambapo Serikali ilitumia Maabara za Mamlaka.

Dk.Mafumiko amefafanua katika mitambo mitano iliyonunuliwa imeongeza ufanisi wa kazi na kuahidi Serikali itaendelea kuwapa vitendea kazi vingine kama mashine na kuweka katika ofisi za Kanda zilizoko mikoani ili kusogeza huduma karibu na wananchi pamoja na kupunguza mzigo kwa maabara zilizopo Makao Makuu.

Amesema kuwa Serikali katika awamu ya tano imesaidia kuwaongezea idadi ya wafanyakazi kutoka 167 waliokuwepo mwaka 2016 hadi kufikia 290 Desemba mwaka 2018 ikiwa ni sehemu ya kuongeza ufanisi wa utendaji ndani ya taasisi hiyo.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Ocean Road Dk.Julius Mwaiselege amesema kuwa Serikali imewekeza katika taasisi hiyo katika mashine ya uchunguzi wa saratani saratani mbalimbali.

Amesema kuwa wameongeza mapato kutoka Sh.bilioni saba hadi Sh.bilioni 13 kwa kipindi mwaka 2015 hadi 2018.

Dk.Mwaiselege amesema kuwa wataendelea kutoa huduma bora katika hospitali hiyo ili kuokoa watanzania wenye saratani.

Kaimu Meneja wa Kitengo cha DNA Kaisunga Brassy akizungumza na maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya wakati walipotembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Vielelezo kwa ajili ya uchunguzi wa vinasaba DNA katika mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakiendelea na uchunguzi wakati Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara walipotembelea ofisi hiyo.
Mkemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali(GCLA) Dkt Fidelice Mafumiko akizungumza na maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakati walipotembelea ofisi ya Mamlaka hiyo katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais wa Awamu ya Tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli. 
Mwakilishi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Akizungumza na katika taasisi ya saratani ya Ocean Road katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya a Afya inayofanywa na maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kuangalia uwekezaji uliofanywa na serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali(GCLA) George Kisiga akizungumza na maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo pamoja na waandishi habari waliopo katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya ikiwa ni kuangalia uwekezaji uliofanywa na serikali katika utoaji wa huduma kwa wananchi katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais wa Awamu ya Tano Dkt.John Pombe Magufuli.
Moja ya mashine ya LCMS/MS iliyopo katika Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ambayo uwezo wake inatoa matokeo ndani ya dakika 40 ambayo imenunuliwa kwa sh. bilioni 1.6
Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto wakiwa katika moja ya Maabara ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...