Anaandika Dixon Busagaga,Moshi .

MWANAMITINDO na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss Universe, Marisela De Montecristo amewasili nchini usiku wa kuamkia kwa lengo la kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Ngorongoro zilizopo mkoani Arusha. 

Marisela amewasili usiku wa jana katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege ya shrike la ndege la KLM na kupokelewa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira. 

Akizungumza na Waandishi wa habari Marisela ambaye ni raia wa nchi ya El Salvador aliyehamia Los Angels, Marekani amesema lengo la kuja nchini kutembelea vivutio vya utalii ni pamoja na kuangalia fursa mpya ipatikanayo katika sekta ya Utalii Duniani pamoja na kuvitangaza. 

Marisela ambaye ameongozana na mchumba wake pamoja na mama yake mzazi akaeleza nia yake ya kuja Tanzania ikiwemo kukuza uchumi kupitia utalii ,elimu kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania . Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna mghwira amesema hii ni fursa adhimu ambayo nchi nyingi zenye vivutio vya utalii zimekua zikitamani hasa kwa kutembelewa na watu mashuhuri Kwani kupitia kwao inasaidia kutangaza utalii Duniani. Mwenyeji wa ugeni huo ,Dennis Meela akaeleza namna alivyo fanya ushawishi kwa Mwanamitindo huyo hadi kuamua kuja Tanzania. 

Mwanamitindi huyo kesho (Januari 18) ataanza safari ya kwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ambako atakaa hapo kwa siku moja na baadae kuelekea Ngorongoro ambako atashuhudia maajabu ya wanyama katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Bonde la ufa la Ngorongoro (Ngongoro Creator).” Mwanamitindo huyo anakuja kujifunza baadhi ya vivutio anavyotaka kuvitumia kutangaza utalii wa Tanzania kimataifa akiwa ameongozana na na kundi la watu wanne akiwemo mama yake mzazi na mpenzi wake ambaye ni Mwanasheria nguli nchini Marekani. 

Baada ya safari ya siku mbili katika hifadhi hizo atarejea Moshi Januari 22 na kutembelea moja ya kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kuona namna ya kuweza kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu. Mwaka jana Merisela ameshiriki mashindano ya ulimbwende nchini El Salvador na kufanikiwa kutwaa taji la hilo (Miss El Salvador 2018). 

Pia amewahi kushiriki mashindano ya Best National Costumes na kufanikiwa kushika nafasi ya pili ambapo nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Brazili na ya tatu Panama. Merisela anamiliki Taasisi binafsi ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini Marekani.

 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akiwa na Mwanamitindo  na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss Universe, Marisela De Montecristo,mara baada ya kuwasili nchini usiku wa kuamkia jana kwa lengo la kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Ngorongoro zilizopo mkoani Arusha. Marisela amewasili usiku wa jana katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege ya shrike la ndege la KLM .

 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akizungumza jambo na na Mwanamitindo  na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss Universe, Marisela De Montecristo,mara baada ya kuwasili nchini usiku wa kuamkia jana kwa lengo la kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Ngorongoro zilizopo mkoani Arusha. Marisela amewasili usiku wa jana katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege ya shrike la ndege la KLM 


 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akimpokea Mwanamitindo  na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss Universe, Marisela De Montecristo,mara baada ya kuwasili nchini usiku wa kuamkia jana kwa lengo la kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Ngorongoro zilizopo mkoani Arusha. Marisela amewasili usiku wa jana katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege ya shrike la ndege la KLM .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...