Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia kesi ya utakatishaji fedha  aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya, na wenzake wawili kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea na kesi  hiyo.

Pia Mahakama hiyo imemfutia kesi mfanyabiashara aliyewahi kutajwa na Rais John Magufuli kuiibia serikali Mil.7 kwa dakika, Mohamed Yusufal na wenzake kwa sababu DPP hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kesi hizo zote zimefutwa mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mbando na Salim Ally, baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Hashim Ngole kueleza kuwa kesi hizo leo zilikuja kwa  kutajwa.

Wakili Ngole ameeleza kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashauri hayo kwa kutumia kifungu cha 91(1) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 marejeo ya mwaka 2002.

Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Mmbando ameziondoa kesi hizo mbili.
Hata hivyo, baada ya kutoa uamuzi huo washtakiwa wote walikamatwa na sasa wako ndani ya ukumbi wa wazi wa mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando wakisomewa mashtaka mapya.

 Kitilya anashtakiwa pamoja na aliyekuwa miss Tanzania (1996), Shose Sinare na Ofisa wa benk ya Stanbic Sioi Solomon.

Katika kesi ya awali, washtakiwa walikabiliwa na makosa ya utakatishaji fedha, kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha Dola za Marekani Milion 6 katika akaunti tofauti tofauti  za benki ambapo inadaiwa walitenda makosa hayo kati ya March 2013 na September 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...