*Gulamali azishukuru  TAMISEMI na Wizara ya Elimu kwa kutoa shilingi milioni 480 kwa sekta ya Elimu.

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MBUNGE wa Manonga Seif Gulamali kwa niaba ya wananchi wa jimbo la manonga na Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ametoa shukrani za dhati kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kuunga mkono jitihada za maendeleo nchini na kwa jimbo la Manonga.

Gulamali amesema kuwa uongozi wa awamu ya tano chini Rais Magufuli umegusa maisha ya watu wengi sana wakiwemo wana Manonga ambapo sekta za afya, barabara, elimu, kilimo na viwanda zimeimarika zaidi na ujenzi wa taifa upo katika kasi ambayo manufaa yake ni kwa kila mmoja.

Amesema kuwa wanamanonga wanamtakia Rais Magufuli afya njema na kulipeleka taifa mbele zaidi. Wakati huo huo Gulamali ameishukuru TAMISEMI na Wizara ya Elimu kwa kutoa jumla ya shilingi milioni 480 kwa ajili ya kuimarisha sekta ya Elimu jimboni humo.

Amesema kuwa shule ya Sekondari Choma itapata jumla ya shilingi milioni 190 ambazo zitatumika katika ujenzi wa madarasa 2 na mabweni 2. Pia katika shule ya Sekondari ya Mwisi shilingi milioni 190 zitatolewa ambazo zitatumika katika ujenzi wa madarasa 2 na mabweni 2 ili  kuweza kuchukua wanafuzi wengi zaidi.

Pia shule ya Sekondari Ziba itapata shilingi milioni 100 ambazo zitatumika katika ujenzi wa bwalo la chakula. Gulamali amewahakikishia wanamanonga kuwa nguvu iliyopo katika kuboresha sekta za Elimu, Afya na miundombinu haitalega na amewataka kuwa na umoja na ushirikiano katika kuleta maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...