Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

WIZARA ya Fedha na Mipango kupitia Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) imeandaa warsha kuhusu udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi kwa wadau wa sekta ya fedha nchini.

Lengo la warsha hiyo ni kuendelea kuwakumbusha wadau kuhusu umuhimu wa kulinda mfumo wa fedha wa nchi yetu ili usitumiwe vibaya na wahalifu na watu wasio waaminifu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo kuhusu udhibiti wa utakatishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi, Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Onesmo Makombe alisema tatizo la utakasishaji wa fedha haramu ni tatizo kubwa ulimwenguni kote na katika jamii.

Amesema ni kwasababu ya kuwepo kwa vitendo mbalimbali vya uhalifu vinavyowapatia wahalifu pato haramu. Uhalifu huo ni pamoja na ukwepaji kodi, biashara haramu ya dawa za kulevya, biashara haramu ya watu, biashara haramu ya silaha, rushwa, kughushi, ujangili, uharamia, uvunaji haramu wa magogo, uuzaji wa bidhaa bandia, ujambazi na uporaji

Aidha amebainisha madhara ya utakasishaji wa fedha haramu kuwa ni ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiusalama. Madhara hayo pamoja na uhalifu kuendelea kushamiri kwa uhalifu na wahalifu kujiimarisha; wahalifu kuwa na nguvu kiuchumi.

Pia kuhatarisha utawala wa sheria na usalama kwani uhalifu unaposhamiri na makundi ya uhalifu yanapojiimarisha hupata nguvu na kujaribu kudhibiti vyombo vya au kushindana na vyombo vya dola; kuharibu ushindani wa kibiashara katika uchumi kutokana na wahalifu kuwa na mitaji inayotokana na fedha haramu.

Amefafanua madhara mengine ni wafanyabiashara halali hushindwa kuhimili ushindani; kushusha hadhi ya nchi kimataifa na kusababisha nchi kutonufaika na mfumo wa fedha wa kimataifa; kushusha imani ya wawekezaji na kusababisha uwekezaji kupungua.

"Na wawekezaji wapya kutotaka kuwekeza kutokana na kushamiri kwa uhalifu, wawekezaji huwa na hofu kuwa mitaji na mali zao havitakuwa salama; imani ya washirika wa maendeleo na jumuiya ya kimataifa hupungua na nchi huathirika kiuchumi; kushuka kwa hadhi ya taasisi za fedha na mfumo mzima wa fedha.

"Na nchi kushindwa kufikia malengo ya maendeleo kwani rasilimali huwa mikononi mwa wahalifu wachache badala ya kutumika kutekeleza ajenda pana ya maendeleo ya nchi," amesema Makombe.

Wakati huo huo Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu amewakumbusha washiriki wa warsha hiyo kuendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali kutekeleza wajibu wao wa kisheria kwa uadilifu na uaminifu ili kusaidia katika kubaini wahalifu wanaoweza kutumia mfumo wa fedha wa nchi kutakasisha fedha haramu na kufadhili vitendo vya kigaidi na kuhatarisha usalama wa nchi. 

Warsha hiyo imejumuisha washiriki kutoka benki na taasisi zinazotoa huduma za kibenki na huduma ndogo ndogo za fedha.
Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe akizungumza na Watumishi wa Taasisi Mbalimbali za kifedha nchini
Kamishna Msaidizi ,Huduma za Kompyuta Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Gilbert .R.Nyombi akizungumza na Watumishi wa Taasisi Mbalimbali za kifedha nchini alipokuwa akitoa mada juu ya kudhibiti fedha haramu.
Baaadhi ya Washiriki wa Warsha hiyo wakifatilia mada zilizokuwa zikitolewa na Mtaalamu kutoka FIU Kwa umakinimu.
Washiriki wakiwa katika Makundi kujadili mada zilizowashirishwa na wao kuchangia katika suala zima la utakatishaji fedha kutumia taasisi za kifedha. 
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika Picha ya Pamoja na AmuKamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe 
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika Picha ya Pamoja na AmuKamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...