Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

Timu ya Yanga imekuwa timu ya pili kuondolewa kwenye michuano ya Sportpesa baada ya kukubali kichapo cha goli 3-2 kutoka kwa Kariobang Sharks.

Mchezo huo wa pili ulizikutanisha timu hizo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na KK Sharks kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali.

Ilichukua dakika 10 kwa KK Sharks kuandika goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wake Duke Abuye.Yanga waliendelea kupambana kupata goli la kusawazisha wakishindwa nafasi walizozipata na kuwapa nafasi wapinzani wao kufanya mashmbulizi ya mara kwa mara langoni mwao.

Katika dakika ya 37 mchezaji wa KK Sharks anaipatia timu yake goli la pili na kuelekea mapumziko wakiwa wanaongoza kwa jumla ya goli 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kutafuta namna ya kufanya marekebisho ya makosa ya kipindi cha kwanza kwa kusaka magoli ya kusawazisha.

Mshambuliaji wa Yanga Amisi Tambwe anaipatia Yanga goli la kwanza kwenye dakika ya 86 ya kipindi cha pili na haikuchukua mda mrefu Duke Abuye wa KK Sharks anaiandikia Timu yake goli la 3 dakika za nyongeza na kupeleka simanzi zaidi kwa Yanga.

Dakika ya 90+5 Tambwe anaipatia timu yake goli la 2 na kupelekea matokeo kuwa 3-2. Mpaka dakika 90 za mtanange huo unamalizika Yanga inakuwa timu ya pili baada ya Singida United kuaga mashindano hayo kwa jumla ya goli 3-2.

Michuano hiyo inaendelea tena kesho kwa Gor Mahia kuumana na Mbao Fc huku Simba wakishuka dimbani kuvaana na AFC Leopard na mshindi wa michuano hii atacheza na timu ya Everton kutoka Ligi Kuu Uingereza zote zikiwa ni timu zinazodhaminiwa na kampuni ya ubashiri Sportpesa.
Wachezaji wa Kariobang Sharks wakiwa wanashaangalia baada y kufanikiwa kuiondoa Yanga kwenye hatua ya robo fainali ya Michuano ya Sportpesa leo katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...