Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amewaambia Majaji 15 wa Mahakama Kuu ambao wameapishwa siku za karibuni kwamba wanatakiwa kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika utoaji wa haki.

Majaji hao ambao waliteuliwa na kuapishwa na Rais John Magufuli Januari 27, mwaka huu ni Cyprian Mkeha, Dunstan Ndunguru, Seif Kulita, Dk Ntemi Kilikamajenga, Zepherine Galeba, Dk Juliana Masabo, Mustaphafa Ismail, Upendo Madeha, Willibard Mashauri, Yohane Masara , Dk Lilian Mongella, Fahamu Mtulya, John Kahyonza, Athuman Kirati na Suzan Mkapa,

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa majaji hao leo jijini Dar es Salaam katika Kituo cha Mafunzo Kisutu, Dar es Salaam Jaji Profesa Juma amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwakaribisha mahakamani ili kujua mambo ya msingi watakayokumbana nayo wakiwa mahakamani.

Profesa Juma amesema mbali ya kuwakaribisha pia wanawakumbusha kuwa ingawa wao ni Majaji lakini wanafanya kazi katika nchi ya Tanzania.
Amefafanua majaji wa zamani walikuwa hawapendi kurudishwa madarasani kwa ajili ya kusoma lakini kwa dunia ya sasa, masomo ambayo wanafunzi wanasoma kwenye shule ya sheria wanapofika kazini kuna kuwa na mabadiliko makubwa.

Ameongeza kuwa bila kuwa na elimu endelevu ikiwemo kujua teknolojia ya habari inaendaje, na changamoto zake majaji hao watakuwa wanabaki nyuma.Profesa Juma amesema "Hatutaki Majaji wetu wabaki nyuma bali wawe wa kisasa ili kushughulikia changamoto zinazoikabili jamii yetu."

Pia miongoni mwa maeneo ya kimkakati ya Mahakama ni maadili katika kujenga imani ya wananchi kuweza kuiamini mahakama, kushughulikia umalizaji wa kesi mapema na kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

"Dunia imebadilika kutokana na maendeleo ya Tehama na kwamba tumefanikiwa kuwa na kituo hicho cha mafunzo Kisutu ambacho kina mitambo ya kisasa ya kukusanya ushahidi kwa mashahidi wanaokuwa sehemu za mbali," amesema.

Kwa upande wake Jaji Kiongozi, Dk.Eliezer Feleshi amesema kwamba Mahakama imeweka mkakati wa kutoa mafunzo kwa watumishi wanaojiunga na mahakama, mahakimu na majaji.Amesema mafunzo hayo ni fursa kwa Majaji ambao wameteuliwa kwa sifa zao, kupitisha maeneo mbalimbali yanayohusiana na utoaji haki.

Pia amesema Mahakama inafanya maboresho mbalimbali na Majaji hao wataongeza ujuzi wao, hivyo wanapaswa kutambua kuwa wao ni viongozi na kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria na kutoa haki.Jaji Dk.Feleshi amesema majaji hao wanaungana na wengine ambao wameanza kazi ya utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya maboresho ya mahakama.

Wakati huo huo Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Jaji Paul Kihwelo amesema mafunzo hayo yatafanyika kwa wiki tatu kwenye kituo cha Mafunzo ya Habari za Kimahakama Kisutu, Dar es Salaam na Lushoto mkoani Tanga.

Pia amesema baadhi ya majaji hao hawakuwahi kufanya kazi za mahakama, hivyo watapata fursa ya watatembelea Mahakama mbalimbali na kujifunza kwa vitendo namna mahakama inavyofanya kazi.Amesema kuwa majaji hao hupata fursa ya kujadili changamoto mbalimbali anazokabiliana nazo Jaji wakati wa kutimiza majukumu yake, kuzingatia maadili ya jaji, kutunza wakati, staha, weredi na usikivu.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...