Mashuka yenye urembo wa maua ya kushonwa na rangi za kuvutia yamening'inizwa pembezoni mwa barabara na nje ya nyumba kama uzio, ni ishara inayoweza kukujulisha kuwa umefika Kigoma.

Ni katika mji mkongwe wa Ujiji uliopo Kigoma Kaskazini, Magharibi mwa Tanzania eneo ambalo ni zaidi ya kilomita 1000 kutoka jiji la kibiashara la Dar es Salaam.

Waswahili wanasema usilolijua ni sawa na usiku wa giza, maana uwepo wa mashuka hayo si kwa ajili ya kujipatia kipato tu bali ni mila na desturi kama lilivyo vazi la khanga.Na kuchagua mashuka mazuri, unahitaji usaidi wa kujua majina na ujumbe uliopo kwenye shuka unalolichagua.

Kila shuka lina jina lake, ambapo mengi yamebatizwa majina ya watu maarufu, wakiwemo viongozi wa kisiasa kama Mbunge wa mkoa huo Zitto Kabwe, Obama, Magufuli, Lowasa, Wema Sepetu na mengine mengi.

Huku majina mengine yakiwasilisha wanyama na vitu mbalimbali kama vile Pundamilia, Tausi, Nanasi, samaki wa kigoma, mwanamke mazingira, jumba la maneno, msala, pembe la ng'ombe, mwiba na kapu la kigoma.

Joslyn Anthon alianza kufuma tangu mwaka 1996 na anasema biashara hii inamfanya mwanamke ashughulike na kupata kipato.

"Huu ni utamaduni wetu kigoma , ukitafuta shuka za kufuma utazipata kigoma, Wanawake wa mkoa huu ni karibu wote wanajua kufuma mashuka haya na jambo muhimu kwao si kujipatia kipato tu bali ni kutunza mila na desturi yao."

KUENDELEA KUSOMA MAKALA HII BOFYA BBC swahili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...