Na Ripota Wetu
KLABU ya Soka ya Juventus wanajipanga kutoa kitita cha pauni milioni 175 ili kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah(26). Taarifa kuhusu Juventus kujiandaa kumsajili mchezaji huyo wa Liverpool ambaye kwa sasa yupo kwenye ubora zinatokana na tetesi ambazo zimebainika kuwepo kwa mpango huo.

Wakati kukiwa na tetesi hizo, pia tetesi nyingine katika anga la soka zinaeleza kuwa hatma ya Maurizio Sarri kama kocha wa Chelsea utaamuliwa ndani ya wiki mbili zijazo.Tetesi hizo ni kwa mujibu wa Telegraph. Hata hivyo wakati ikisubiriwa hatma ya kocha huyo, inaelezwa kuwa wachezaji wa Chelsea walifanya kikao maalum cha 'kurekebishana' katika uwanja wao wa mazoezi wa Cobham jana Jumatatu kutokana na kipigo walichopata cha 6-0 dhidi ya Manchester City. (Mail)

Naye Kocha wa Derby Frank Lampard amepuuzia uvumi kuwa huenda akarithi mikoba ya Maurizio Sarri endapo Chelsea itaamua kumfukuza. (Evening Standard) Wakati huo huo kuna tetesi zinaeleza kuwa Beki wa Tottenham Juan Foyth mwenye umri wa miaka 21 amefichua kuwa alikataa kujiunga na klabu ya Paris Saint- Germain ili ajiunge na Spurs mwaka 2017. Tetesi za beki huyo zimetolewa na Goal. Tetesi nyingine kwenye soka zinadai kuwa Barcelona wamefikia makubaliano na klabu ya Eintracht Frankfurt kumsajili streka wao raia wa Serbia Luka Jovic, 21, mwishoni mwa msimu. (Diario Sport)

Wakati mshambuliaji wa Juventus raia wa Argentina Paulo Dybala, 25, anakaribia kufikia makubaliano ya kuhamia Real Madrid mwishoni mwa msimu. (AS) Kwa upande wa Manchester United wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa Paris Saint-Germain Adrien Rabiot(23) mwishoni mwa msimu. (AS - via Mirror).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...