Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)  kesho, inatarajia kufanyia marekebisho hati ya mashtaka dhidi ya kesi ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni 14 inayomkabili mfanyabiashara  maarufu aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa alikuwa akiibia Serikali takribani Sh. Milioni Saba kwa dakika, Mohamed Yusufali na mfanyakazi wake Arital Maliwala. Kwa kumuongeza mshtakiwa mmoja. 

Wakili wa Serikali kutoka Takukuru,  Leornard Swai ameeleza mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu kuwa,  kesi hiyo leo imekuja kwa ajili ya kutajwa na pia walitarajia kufanyia mabadiliko hati ya mashtaka  hata hivyo wamekwama kidogo hivyo wanaomba shauli hilo lije kesho ili wafanye mabadiriko hayo. 

Kufuatia maelezo hayo Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi kesho kwa ajili ya kufanyika kwa mabadiliko hayo. 

Yusufali na mfanyakazi wake Maliwala wanaokabiliwa na mashtaka 601 likiwemo hilo la kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh.  bilioni 14.

Katika mashtaka hayo, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kughushi, kuwasilisha taarifa za mwezi za mahesabu ya uongo kwa Mamalaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), kukwepa kodi na kuisababishia serikali hasara ya sh. 14,987,707,044.58.


Katika shtaka la kuisababishia serikali hasara, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa la kusabisha hasara ambayo imetokana na kukwepa kodi ya serikali kwa kipindi cha mwaka 2008 hadi 2015 kupitia kampuni ya Pamplant ltd iliyokuwa inamilikiwa na mshtakiwa Yusufali ambapo mshtakiwa Paliwala alikuwa mfanyakazi wake.

Inadaiwa kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo wakiwa wanatumia stakabadhi za kughushi pamoja na kutumia makampuni ya kughushi wakidai kuwa wamenunua vitu kutoka katika makampuni mbalimbali wakati wakijua baadhi ya kampuni hizo ni za kughushi huku zikiwa hazijasajiliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brella).

Pia imedaiwa kampuni hizo zina majina ya kampuni ambazo hazapo brella na zina namba  za usajili ambazo brella haijazifikia huku pia wakiwa wanaghushi stakabadhi za malipo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...