Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma wakimfanyia mgonjwa uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (coronary angiogram) kwa kutumia mtambo wa Cathlab. Mtambo huo wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo umeanza kufanya kazi kwa mara ya kwanza leo na kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa watano.




Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kumaliza kufanya uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (coronary angiogram) kwa mgonjwa wa kwanza kwa kutumia mtambo wa Cathlab. Mtambo huo wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo umeanza kufanya kazi leo na kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa watano.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwafundisha wataalamu wa afya wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma kuhusu madhara ya moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure) kabla ya kuanza kwa uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (coronary angiogram) kwa wagonjwa kupitia mtambo wa Cathlab. Mtambo huo wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo umeanza kufanya kazi leo na kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa watano.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma pamoja na timu ya wataalamu wa Taasisi hiyo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Catheterization) kupitia tundu dogo linalitobolewa kwenye paja. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa BMH Dkt. Alphonce Chandika.Picha na JKCI



MADAKTARI bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) wameanza kutoa huduma ya uchunguzi na uzibuaji wa mishipa ya damu ya moyo iliyoziba kwa kutumia mtambo wa Cathlab.

Jopo la mabingwa waliotoa huduma hiyo kwa mara ya kwanza leo tarehe 11/02/2019 katika Hospitali hiyo limeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI prof. Mohamed Janabi pia ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo leo Prof. Janabi alisema kwa siku ya kwanza wamefanya uchunguzi kwa wagonjwa watano ambapo wawili kati yao mishipa yao ya damu imeziba na inatakiwa kuzibuliwa.

“Madaktari wa JKCI na BMH kwa mara ya kwanza tumeweza kufanya uchunguzi kwa wagonjwa ili kuangalia mishipa iliyoziba kwa kutumia mtambo wa Cathlab ambao serikali imewekeza fedha nyingi kuununua na kuufunga,” alisema.Alisema adhima ya serikali ni kuwasaidia wagonjwa wenye matatizo ya moyo, hasa matundu na kuziba kwa mishipa ya damu, kupata huduma hizi kwa karibu.

Alisema mtambo wa cathalab uliofungwa BMH ni wa kisasa zaidi na kwamba unao uwezo wa kuchunguza mishipa iliyoziba kwenye moyo bali hata mishipa ya damu iliyoziba kichwani na miguuni.Profesa Janabi alisema huo ni mwanzo wa safari ya kusogeza huduma hiyo karibu zaidi na wananchi na kwamba zitakapoimarika BMH zitaweza kusogezwa maeneo mengine nchini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa BMH na Daktari Bingwa wa Upasuaji, Dk. Alphonse Chandika, alisema kuanza kutolewa kwa huduma hiyo ni hatua kubwa mno kwa hospitali hiyo.“Hii itakuwa huduma endelevu, nawasihi watanzania Serikali imedhamiria wanakuwa na afya njema na matibabu yote waliyokuwa wanayafuata nje ya nchi, sasa watapata hapa nchini,” alisema.


kizungumza Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo BMH, Willfredius Rutahoile alisema kila mwezi huwa wanapokea wagonjwa wapatao 300 wanaohudhuria kliniki ya moyo, hadi sasa wagonjwa wapatao 63 wanasubiri huduma hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...