Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes wametoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu zinazoshiriki ligi ya mpira wa miguu iliyoandaliwa na jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam inayojulikana Kamanda Cup. Ligi hiyo imeandaliwa mahususi kw ajili ya kuhamasisha elimu ya Usalama barabarani.

Miongoni mwa vifaa ambavyo vimetolewa na StarTimes ni bendera za Kona (corner flag) 4, nyavu za golini (goalkeeper nets), sare za timu, Mipira 12, Saa za refarii, Vipenga, Vitambaa vya Kapteni (Captain Armbands) na Kadi za Refarii. Vifaa hivyo vimekabidhiwa na Afisa Uhusiano wa Kampuni hiyo Samwel Gisayi na kupokewa na Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Ubungo Bi. Fatuma Kiberiti.

“Mara zote tunapenda kujishughulisha na shughuli za Kijamii na hiki ni kielelezo tosha cha nia yetu hiyo. Elimu ya Usalama barabarani ni muhimu sana kwa jamii nzima na sisi kama StarTimes tuko bega kwa bega na serikali katika kuhakikisha hilo”. Samwel Gisayi, Afisa Uhusiano StarTimes.
“Michezo inaleta umoja na utimamu wa afya, ni matumaini yetu msaada tuliotoa utakuwa na faida iliyokusudiwa ambayo ni kuboresha jamii inayotuzunguka ili tunapotumia barabara zetu kila mmoja awe na uwezo wa kutimiza wajibu wake. Sisi StarTimes tumeshiriki kwa nafasi yetu” aliongeza.

Naye mratibu wa ligi hiyo Mpalule Shabani alitoa shukurani kwa Kampuni hiyo kwa kukubali kuchangia vifaa hivyo huku akitoa wito kwa timu zinazoshiriki kujiandaa kikamilifu kwani ligi ni ngumu hasa ukizingatia kuwa ni mtoano. “Ligi inashirikisha jumla ya timu 128 kutoka majimbo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam, leo tuko Sinza wiki ijayo tutatangaza tutakuwa wapi. Timu 128 zinacheza kutafuta 64 bora, mashindano haya ni mtoano hivyo kila timu inatakiwa kujipanga ipasavyo. Mashindano ni magumu.” Mpalula Shabani.
Afisa Mahusiano wa Star Media (T) Ltd,  Samwel Gisayi akikabidhi vifaa vya michezo kwa Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Bi. Fatuma Kiberiti. Vifaa hivyo vitasaidia kufanikisha Ligi ya Mpira wa miguu iliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dar es Salaam kwa lengo la kueneza elimu ya Usalama Barabarani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...