Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kushoto akizungumza wakati alipofanya ziara yake wilaya ya Tanga kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi. 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi k,ushoto anayemsikiliza kwa umakini ni Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akisistiza jambo wakati wa ziara hiyo 
Afisa Raslimali watu wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Haika Ndalama akizungumza wakati wa ziara hiyo 
Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa katika akitazama mitambo ya uzalishaji wa maji Moye Jijini Tanga kushoto ni nMkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia ni Msimamizi wa shughuli za Uzalishaji Maji katika kituo cha kuzalishia Maji Mabayani Faraji Nyoni 
Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa mwenye kofia katikati akiangalia namna maji kwenye kituo cha Kuzalishia maji cha Mabayani Jijini Tanga wakati alipokitembelea ikiwa ni ziara yake kulia ni msimamizi wa shughuli za Uzalishaji Maji katika kituo cha kuzalishia Maji Mabayani Faraji Nyoni,Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly,Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said 
Msimamizi wa shughuli za Uzalishaji Maji katika kituo cha kuzalishia Maji Mabayani Faraji Nyoni kushoto akimuonyesha Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa jambo wakati wa ziara hiyo 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akimuelezea jambo Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kulia wakati alipotembelea kituo hicho 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akimuelezea jambo Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kulia wakati wakitoka kwenye kituo hicho



MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imetakiwa kuhakikisha wanalilinda bwawa la maji la mabayani kwa kuliwekea mipaka ili kuepusha kuvamiwa na wananchi wanaoishi karibu nalo. 

Hayo yalisemwa na Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa wakati alipolitembelea bwawa hilo ikiwa ni ziara yake mkoani Tanga ambapo alisema hilo linatokana na bwawa hilo kuwa ndio tegemezi kubwa kwa mji wa Tanga na maeneo ya karibu. 

Alisema ni muhimu kulindwa kwa eneo hilo la kwenye mabwawa hayo ikiwemo kutumia sheria za mita 500 kutoka kwenye bwawa hilo ili lisiweze kuvamikwa na wananchi ambao kila siku wamekuwa wakisaka ardhi kwa ajili ya matumizi. 

“Ndugu zangu wataalamu jambo kubwa ni kuhakikisha wanalilinda eneo hili la kwenye mabwawa hayo lakini pia sheria inasema mita 500 au waziri anaweza kutoa maelekezo ni muhimu kupata mita 500 zinafaa kubwa hasa maeneo ya chini kabla ya wananchi hawajavamia kwani bwawa linaweza kupasuka na kusababisha watu kupoteza maisha”Alisema Waziri Mbarawa. 

Alisema lazima kuwepo kwa mita hizo kutokana na kwamba iwapo wananchi wataishi karibu sana na na bwawa hili ikitokea siku bwawa limepasuka maji yanaweza kusambaa sehemu kubwa mifano ipo mingi mabwawa yanapasuka na watu kupoteza maisha .“Maeneo ya chini ya mabwawa wananchi waiishi jambo ambalo ni hatari kwani bwawa linapopasuka kuna madhara makubwa yanaweza kuwakumba yakiwemo ya kupoteza maisha ….lakini pia ni vema kabla ya wananchi hawajavamia tuweke alama zetu za mabwawa hasa sasa hivi tusije kukaa kama tukapata shida kama tunazozipata bwawa la mindu”Alisema Waziri Proffesa Mbarawa. 

“Bwawa hili lazima lilindwe liwekewe mipaka wajuia wapi mwisho wa bwawa kwani bila kufanya hivyo tukiliacha ardhi kila siku inapungua wananchi wanasaka ardhi hasa kwenye maeneo yenye maji maji hivyo baadae tunaweza kuja kupambana na wananchi kuhusu eneo hilo kama hatutalilinda lakini nashukuru mamlaka kunipa fursa ya kutembelea bwawa la mabayani na ndio tegemezi kubwa kwa mji wa Tanga na maeneo ya karibu kwa ajili ya kupata maji”Alisema 

“Kama alivyosema mtaalamu bwawa lina lita milioni 7.7 kuhifadhi lina uwezo wa kuzalisha maji kwa mji wa Tanga miezi mitano kama ilivyoeleza bila matataizo lakini changamoto kubwa ni magugu hivyo sisi tutaona namna ya kutumia utaalamu wa jinsi ya kuyatoa lengo likiwa bwawa hili liendelea kutumika muda mrefu halina shida lina uwezo mzuri,”Alisema . 

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo,Msimamizi wa shughuli za Uzalishaji Maji katika kituo cha kuzalishia Maji Mabayani Faraji Nyoni bwawa hilo linapokea Mto Zigi unaotoka Amani wilayani Muheza limejengwa mwaka 1976 na 1978 likaanza kazi rasmi kutumika. Alisema bwawa hilo lina kina cha urefu wa mita 24 na lina uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 7.7 maji hayo yana uwezo wa kuwatosheleza miezi mitano hata kama hakuna mvua itakayokuwa ikinyesha kwa kipindi hicho. 

“Lakini changamoto kubwa ni watu wanalima kwenye eneo hilo…watu wanakata miti,bwawa limezunguwa na vijiji vitano na wapo wafugaji hivyo wanakwenda kulishia mtoni bado hairuhusiwi kisheria mamlaka kupitia sheria za vijiji waliunda kamati shirikishi ya vijiji imeweza kusaidia sana kupunguza kidogo tatizo hilo “Alisema . 

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly alisema mpango wa mamlaka hiyo kwa mwaka ujao wa fedha ni kuhakikisha wanabadilisha bomba urefu wa kilomita zaidi ya 50 kuondoa ya zamani ili kuepusha maji kupotea kwa njia ya mivujo. 

Alisema hilo linatokana na mabomba kupasuka mara kwa mara kunakosababishwa na uchakavu wake hivyo wakaona umuhimu wa kjuyabadilisha ili kuweza kuendana na wakati uliopo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...