Na Ripota Wetu
KUNDI la Maseneta wa Republican na Democrats nchini Marekani wamesema
wamefikia makubaliano ya ufadhili wa Serikali kuelekea tarehe ya mwisho
inayotishia kufungwa kwa sehemu fulani ya shughuli za Serikali.
Kwa mujibu wa mtandao wa DW inaeleza kuwa wabunge wanakabiliwa na tarehe ya
mwisho Februari 15 ya ufadhili wa Serikali na kuafikiana na mahitaji ya fedha ya
rais Donald Trump kuhusu ujenzi wa ukuta na Mexico.
Hata hivyo ikiwa tarehe hiyo ya mwisho itafikiwa bila muafaka, Serikali huenda
ikafunga sehemu fulani ya shughuli zake na kuwalazimu mamia kwa maelfu ya
wafanyakazi wa shirikisho kufanya kazi bila ya malipo. Vyombo vya habari vya
Marekani vimemnukuu seneta wa Republican Richard Shelby kuwa kumefikiwa
makubaliano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...