Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Bandari hiyo kwa wafanyabiashara wa Mikoa ya kanda ya Kaskazini waliotembelea na kuvutiwa kupitisha shehena za mizigo yao
Wafanyabiashara hao wakiendelea kupata ufafanuizi wa masuala mbalimbali
 Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akiwa na Katibu tawala Msaidizi wa mkoa wa Kilimanjaro wakitembelea eneo la Bandari ya Tanga

 Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza na wafanyabiashara hao
 Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Bandari nchini Lydia Mallya akizungumza ambapo aliwataka wafanyabiashara hao kutumia bandari hiyo kwani tayari ni bandari ya viwango vya kimataifa.
 Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa wa Kilimanjaro akizungumza kulia ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Kilimanjaro Patrick Shirima akizungumza katika hafla hiyo
 Sehemu ya ujumbe wa wafanyabiashara kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini wakifuatilia nyumba anayefuatilia ni Moni Jarufu PRO wa Bandari ya Tanga akifuatilia mkutano huo
 Wadau mbalimbali nao wakifuatilia ziara hiyo
Sehemu ya wafanyabishara wakifuatilia mkutano huo katikati ni Meneja wa Bohari ya Mafuta ya GBP mkoani Tanga Amour

WAFANYABIASHARA wa Mikoa ya kanda ya Kaskazini wameonesha nia ya kuanza kutumia Bandari ya Tanga kupitisha shehena ya mizigo yao baada ya kuridhishwa na mabadiliko makubwa ya mfumo wa utendaji wa Bandari hiyo.

Wameonesha nia hiyo kwenye mkutano wa siku moja baina ya Uongozi wa mamlaka hiyo na wafanyabiashara hao na wadau mbalimbali kutoka mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Arusha.

Katika mkutano huo wafanyabiashara hao waliongozwa na viongozi wa vyama vya Chemba za Biashara,Kilimo na Viwanda(TCCIA),Katibu tawala Msaidizi wa oa wa Kilimanjaro na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini na uongozi wa mamlaka ya Bandari Tanga.

Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama amefafanua kuwa katika kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma bora kwa wateja wake imeboresha miundombinu na mifumo ya utendaji na ulinzi katika bandari hiyo.

Amesema kuwa kutokana na maboresho hayo taratibu za uchukuaji wa mizigo zinatumia muda mchache tofauti na awali kutokana mamlaka zote za serikali zinazohusika na Bandari zipo kwenye jengo moja.

" Tunataka kuwaondoa hofu wafanyabiashara kuwa sasa hivi Bandari ya Tanga ni nzuri,salama kwa mizigo na ni ya uhakika kutokana tumeboresha kuanzia mifumo ya ulinzi,miundombinu,utendaji kazi na Tehama" alisema.

Alieongeza " Kutokana na maboresho hayo ikiwa mteja atakamilisha taratibu zote za uchukuaji wa mizigo basi kuanzia mizigo kufika bandarini atatumia siku tatu tu" alisema.

Katika kusogeza huduma zake kwa wateja wa mikoa ya Kaskazini ya Kilimanjaro na Arusha tayari uongozi wa mkoa wa Arusha kupitia mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo ametoa eneo lenye ukubwa wa ekari 500 eneo la Malula katika wilaya ya Arumeru kwa ajili ya ujenzi wa bandari kavu.

" Wafanyabiashara wa Arusha na Kilimanjaro mtakuwa hamna haja ya kuja hadi Tanga kuchukua mizigo mtakuwa mnasubiri mizigo yenu huko huko Arusha sisi tunamiambia gharama zetu tu mnalipia moja kwa moja na sisi tutajuana na Shirika la Reli( TRC) ambao tunategemea ukarabati wa reli ukikamilika uwatumie wao" alisema.

Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Bandari nchini Lydia Mallya aliwasihi wafanyabiashara hao kutumia bandari hiyo kwani tayari ni bandari ya viwango vya kimataifa.

Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Kilimanjaro Patrick Shirima amesema kuwa waliikimbia Bandari ya Tanga na kuhamia Bandari ya Mombasa nchini Kenya kutokana na urasimu uliokuwa unafanywa na taasisi za serikali zilizokuwa zinahusika na utoaji wa mizigo jambo ambalo lilikuwa linachelewesha mizigo.

" Leo mmetufumbua masikio kusikia haya mabadiliko sasa tunaahidi kutumia Bandari yetu kwa ajili ya kuingizia mapato serikali yetu, kwani neno Bandari ya Tanga tuliisahau kabisa" alisema.

Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Arusha Walter Maeda aliongeza kuwa kwa wafanyabiashara wa Arusha wanafahamu kuwa kikwazo kikubwa katika bandari ya Tanga ni taasisi za serikali katika kuchelewesha mizigo ndiyo maana waliachana nayo.

" Sisi tuliikimbia Bandari ya Tanga na kuamua kutumia Bandari ya Mombasa kutokana na nenda rudi zilizokuwa zinafanywa na TRA,TFDA,TBS kwa kweli walikuwa hawana ushirikiano mzuri hali iliyotuletea tabu sisi wafanyabiashara " alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...