*Ni baada ya eneo la awali walilolipata
la kuambiwa kuna shughuli nyingine itafanyika
*Ilikuwa lifanyike viwanja vya Posta
Kijitonyama Aprili 21, 2019
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii.
KAMATI ya Tamasha la Pasaka chini ya
Msama Promotion limesema kwa sasa bado linaendelea kutafuta eneo la kufanyia
tamasha hilo katika Jiji la Dar es Salaam baada ya eneo la awali kupangiwa
shughuli nyingine.
Awali tamasha la Pasaka kwa mwaka huu wa 2019
lilipangwa kufanyika eneo la Viwanja vya Posta Kijitonyoma jijini Dar es Salaam
Aprili 21, lakini Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo imepata maelekezo kuwa
eneo hilo eti limepangiwa shughuli nyingine, hivyo wameanza kutafuta eneo
jingine.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama amewaambia waandishi wa habari
baada ya kuambiwa eneo hilo siku ya Aprili 21 kutakuwa na kazi nyingine, kamati
imeanza kutafuta eneo jingine hasa kwa kuzingatia tamasha hilo kwa mwaka huu
linatakiwa kuanzia katika Jiji hilo.
“Mwaka huu kamati ya maandalizi ya
tamasha la Pasaka liliamua kuwa tuanze jijini Dar es Salaam katika viwanja vya
Posta, hata hivyo tumeambiwa kuwa siku hiyo kutakuwa na shughuli
nyingine.Kamati imeanza kutafuta eneo jingine ili kuhakikisha tamasha hilo
linafanyika Dar es Salaam.
“Kuna maeneo mawili ambayo tunaendelea
kuyafuatilia kwa ajili ya kufanikisha tamasha la Pasaka kwa Mkoa wa Dar es
Salaam.Hata hivyo kwa sasa naomba nisiyataje kwani bado mazungumzo kati ya
kamati yetu na wahusika yanaendelea na tutakapofanikiwa tutaeleza ni
wapi,”amesema Msama.
Amesisitiza ukweli kwa Dar es Salaam
tamasha la Pasaka halijafanyika kwa muda mrefu sana, hivyo walioona mwaka huu
lifanyike na ukweli bado hawajakata tamaa kwani wanaamini litafanyika kama
ambavyo wamekusudia na pale itakaposhindika basi tamasha hilo litaanzia mkoani
na kisha wataangalia namna nyingine ya kulifanyia na Dar.Msama amesema ni matumaini yake kuwa wenye kutoa kibali cha
kutoa maeneo ya kufanyia tamasha hilo watatoa kibali kwani mazungumzo
yanaendelea vizuri.
Kuhusu tamasha hilo, Msama amesema
malengo yake ni yale yale ya kuliombea Taifa ili liendelee kuwa na amani pamoja
na kufanya maombi kumuombea Rais wetu mpendwa Dk.John Magufuli ili aendelee
kuwa na afya njema na hatimaye kuendelea kuwatumikia Watanzaia.
“Kuna mambo makubwa ambayo Rais wetu
ameyafanya ndani ya kipindi kifupi, kuna miradi mikubwa ya maendeleo inaendelea
kutekelezwa ukiwemo mradi wa reli ya kisasa ya SGR na ujenzi wa mradi wa kufua umeme katika Mto
Rufiji. Kwa kazi anayoifanya Msama Promotion kupitia tamasha la Pasaka tunaona
ni wakati sahihi kutumia tamasha hilo kuungana na watanzania wengine kumuombea
Rais.
“Pia huu ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali
za mitaa, hivyo Tamasha la Pasaka litajikita katika kuiombea nchi yetu iendelee
kuwa na amani na kuvuka salama kwenye uchaguzi huu wa Serikali za mitaa.Tamasha
la Pasaka baada ya kuanza jijini Dar es Salaam tutakwenda na mikoa
mingine,”amesema Msama.
Kwa upande wake Mmoja wa Waratibu wa Tamasha la Pasaka
Salehe Mohamed amesema tamasha hilo awali ilikuwa lifanyike Kijitonyama, lakini
kuna shughuli nyingine itafanyika siku hiyo katika eneo hilo.
“
Tunawaomba wananchi wa Dar es Salaam na mikoa mingne ambako tamasha la
Pasaka litafanyika wajitokeze kwa wingi, usalama ni wa kutosha na vyombo vya
ulinzi vimejipanga , hivyo kuhusu usalama ni wa kiwango cha hali ya juu
sana.Tunafahamu nchi yetu kuanzia Amiri Jeshi Mkuu ,Rais Dk.John Magufuli
amehakikisha nchi yetu inakuwa salama.Pia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP
Simon Sirro amekuwa mstari wa mbele kulinda usalama wa raia na mali
zao,”amesema.
Amefafanua kuwa Lazaro kuna mambo mengi ambayo Serikali ya Awamu ya
Tano chini ya Rais Dk.Magufuli yamefanyika na kupitia tamasha la Pasaka wanakila
sababu ya kuwaambia Watanzania mambo mazuri yaliyofanyika nchini kwetu.
“Tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi
kwani badala ya kusimuliwa mambo mazuri yatakayopatikana kwenye tamasha la
Pasaka ni vema wakaja wenyewe ili waone, wasikubali kusimuliwa,”Amesema
Mohamed.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama akizungumza jijini
Dar es Salaam leo ofisini kwakwe Kinondoni kuhusu maandalizi wa tamasha
hilo litakalofanyika Aprili 21 jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama akimsikiliza mmoja wa waratibu wa tamasha hilo Saleh Ali wakati akifafanua zaidi kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 21 jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama akimsikiliza mmoja wa waratibu wa tamasha hilo Saleh Ali wakati akifafanua zaidi kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 21 jijini Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...