Na WAMJW - PWANI

WAZIRI Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amefanya ziara ya kukagua Maendeleo ya ujenzi wa kiwanda vya Dawa cha Vista Pharma Ltd na Kairuki Pharmaceutical Ltd  vinavyoendelea kujengwa kwa kasi katika Mkoa wa Pwani.

Katika ziara hiyo Waziri Ummy alilenga kujionea na kutatua Changamoto zinazowakumba Wawekezaji nchini hususani katika Viwanda vya Dawa ili kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kinachoendelea kupotea kutokana na kuagiza Dawa nje ya nchi.

Waziri Ummy amesema kuwa katika kila Shilingi 100 ambayo Serkkali inatumia kununua Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba, Shilingi 94 inapotea nje ya nchi, ambapo kumalizika kwa Viwanda hivi kutasaidia pesa hiyo kubaki ndani ya nchi na kutumika katika shughuli nyingine za  Maendeleo kwa Wananchi.

"Katika kila Shilingi 100 ambayo Serikali inatumia kununua Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba, Shilingi 94 tunaipeleka nje ya nchi kununua Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba, na ndiomaana nimefanya ziara hii pamoja na viongozi wa Mkoa na kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na Kituo cha uwekezaji ili kuokoa fedha hiyo inayopotea nje ya nchi" alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy aliendele kusema kuwa kumalizika kwa Viwanda hivi kutasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa Dawa za kutosha na kwa bei rahisi, jambo litalosaidia kuimarika kwa huduma za Afya nchini.

 " Dawa kupatikana kwa wingi na kwa bei rahisi na kwa haraka zaidi, kwasababu kuagiza Dawa nje ya nchi MSD anatumia mpaka miezi 6  mpaka ifike Tanzania" alisema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewaagiza Tanesco ndani ya Mkoa kuhakikisha wanaleta huduma ya umeme ndani ya wiki moja ili hatua za mwanzo za ufungaji wa mashine katika Viwanda hivyo uanze Mara moja.

Pia, Waziri Ummy amewaagiza Mamlaka ya Maji Mkoani Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanaleta huduma ya maji ndani ya Machi 15 katika eneo hilo la Viwanda ili kuharakisha shughuli za ujenzi.

Mbali na hayo, Waziri Ummy amewashukuru wawekezaji hao wa Ndani kwa maamuzi mazuri aliyochukua ya kuwekeza katika Viwanda vya Dawa ili kuisaidia Jamii ya Watanzania ambao Dawa bado imekuwa ni changamoto licha ya Jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali katika kukabikiana na changamoto hiyo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Wapili kushoto) akimueleza jambo Mwekezaji wa Vista Pharmaceutical Ltd, wakati wa ziara ya kukagua Maendeleo ya ujenzi wa Viwanda vya Dawa katika unaoendelea katika Mkoa wa Pwani.
 (Picha 1) Muonekano wa Kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Ltd na na Ofisi yake (Picha 2) unaoendelea kujengwa katika Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Wapili kushoto)  akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Assumpter Mshama (wakwanza kushoto), pamoja na Wataaalamu wa masuala ya ujenzi, wakiendelea na ukaguzi wa kiwanda cha Dawa cha Kairuki Pharmaceutical Ltd katika Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani
 Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu baada ya ziara ya kutembelea Viwanda vya Dawa vya  Vista Pharma Ltd na Kairuki pharmaceutical Ltd vinavyojengwa katika Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...