Tanga; March
18th, 2019: Benki
ya Exim mwishoni mwa wiki iliandaa chakula maalum kwa ajili ya wateja wake
jijini Tanga ili kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji
na huduma zitolewazo na benki hiyo katika jiji hilo.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo
viongozi wa kiserikali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wafanyakazi
wa benki hiyo, Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu
wa benki ya Exim Bw Jaffari Matundu
alisema kupitia hafla hiyo walilenga
pia kutoa fursa miongoni mwa wateja hao
ili waweze kufahamiana na kufungua wigo wa kufanya biashara pamoja.
“Pamoja
na kushukuru kwa namna ambayo wateja wetu wamekuwa nasi hadi kufikia mafanikio
ya kuikuaji na ubora wa huduma zetu, hafla hii inatoa fursa kwa wateja wetu pia
kufahamiana wao kwa wao na hivyo kufungua milango ya fursa baina yao,’’ alisema
Matundu.
Alisema
ukuaji wa benki hiyo unaoshuhudiwa kwasasa ni matokeo ya ushirikiano baina yake
na wateja wake ambao kwa kiasi kikubwa wameonyesha imani kubwa kwa benki hiyo
hali ambayo imekuwa ikiiwezesha benki hiyo kubuni huduma bora na rafiki za
kibenki ili kulinda na kurejesha imani hiyo kwa wateja wa benki hiyo.
Tangu
kuanzishwa kwake mwaka 1997 benki hiyo imezidi kujitanua ndani na nje ya nchi
ambapo hivi karibuni ilionesha nia na utayari wa kuinunua rasmi benki ya UBL Tanzania Limited (UBTL)
kwa asilimia 100 baada ya kusainishana barua ya kuonesha nia (Letter of Intent).
“Kwa
muda wote wa uwepo wake ndani na nje ya nchi benki ya Exim imekuwa
ikijipambanua kwa ubora wa huduma ikilenga kujenga thamani ya uwekezaji kwa
wadau wake na kufikia ukuaji wake kwa
kutoa huduma kwa upekee na iliyoboreshwa. Haya yote yamekuwa yakifanikiwa kwa
urahisi sababu utekelezaji wake umekuwa ni jumuishi kwa kuwa unahusisha wadau
wote kwa majadiliano na wateja wetu kama hivi,’’ alisema.
Pamoja
na mambo mengine hafla hiyo ilipambwa na shuhuda mbalimbali kuhusu ubora wa
huduma za benki hiyo kutoka kwa wateja mbalimbali wa benki hiyo.
Meneja
Uendeshaji wa Benki ya Exim Bi Doreen Mcharo (katikati) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki
hiyo wakati wa tafrija ya chakula cha
jioni iliyoandaliwa na benki yaExim kwa
ajili ya wateja wake wa jiji la Tanga
iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo.
Naibu
Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Bw Jaffari Matundu akizungumza
na baadhi ya wateja wa benki hiyo (hawapo pichani) wakati wa tafrija ya chakula cha jioni
iliyoandaliwa na benki yaExim kwa ajili
ya wateja wake wa jiji la Tanga
iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo.
Mmoja wa
wateja wa benki ya Exim Tanzania jijini Tanga Bi Anna Saimo akizungumza kwenye
hafla hiyo.
Mmoja wa
wateja wa benki ya Exim Tanzania jijini Tanga Bw Sifaeli Mafunga akizungumza kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya
wafanyakazi wa banki ya Exim tawi la
Tanga pamoja na Naibu Ofisa Mtendaji
Mkuu wa benki ya Exim Bw Jaffari
Matundu, kwenye picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...