Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walipowasili katika Chuo cha Polisi Kidatu kwa ajili ya ukaguzi na ushauri wa miradi ya serikali.Ziara hiyo imefanyika leo, Mkoani Morogoro. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akifafanua hoja zilizotolewa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa kikao katika Chuo cha Polisi Kidatu kwa ajili ya ukaguzi na ushauri wa miradi ya serikali. Ziara hiyo imefanyika leo, Mkoani Morogoro. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima akifafanua hoja zilizotolewa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa kikao katika Chuo cha Polisi Kidatu kwa ajili ya Ukaguzi na ushauri wa miradi ya serikali. Ziara hiyo imefanyika leo, Mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Shamsi Vuai Nahodha akiuliza swali wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Chuo cha Polisi Kidatu, lengo ikiwa ni kukagua na kutoa ushauri kwa miradi inayotekelezwa na serikali. Ziara hiyo imefanyika leo, Mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna Richard Marika, akifafanua hoja zilizotolewa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa kikao katika Chuo cha Polisi Kidatu kwa ajili ya ukaguzi na ushauri wa miradi ya serikali.Ziara hiyo imefanyika leo, Mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Serikali imetenga jumla ya Shilingi Trilioni 1 .27 kwa ajili ya ukarabati wa Vyuo vitano vya Polisi nchini katika bajeti ya mwaka 2018/2019 gharama hiyo ikijumuisha ukarabati wa majengo ya ofisi, mabweni, makazi ya wakufunzi na maeneo mengine yaliyoanza kuchakaa.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliyotembelea Chuo cha Polisi Kidatu, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhnadisi Hamad Masauni alisema hali ya miundombinu ya majengo kwa vyuo vyote ni chakavu,nia ya Serikali na Jeshi la Polisi ni kukarabati majengo hayo ili yaweze kukidhi mahitaji.

“Tuna vyuo vitano vya polisi nchini;Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Dar es Salaam,Shule ya Polisi Moshi, Chuo cha Polisi Zanzibar, Chuo cha Maafisa Kidatu na Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza hivi vyote vinahitaji ukarabati na tumetenga jumla ya Shilingi Trilioni 1.2 kwa ajili ya ukarabati huo na tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli ameshatoa milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo kimojawapo kati ya hivyo nilivyovitaja” alisema Masauni

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao hicho wajumbe wa kamati hiyo ya bunge waliitaka serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kusimamia mafunzo yanayotolewa vyuoni humo ikiwemo suala la wapelelezi kubambikia kesi wananchi ikiwa ni kinyume na wanchofundishwa vyuoni huku Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mussa Azzan Zungu akiitaka serikali kuwachukulia hatua askari polisi wachache wanaolichafua jeshi na kuivunjia heshima nchi kwa matendo yao ambayo yako kinyume na maadili.

“suala la kubambikiwa kesi lipo , natoa wito kwa serikali kuwachukulia hatua askari dhidi ya tuhuma hizo ambao ni wachache wanakiuka taratibu na ueledi katika shughuli zao za kuhudumia wananchi” alisema Zungu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...