Mmoja wa washukiwa ana historia ya tuhuma za mauaji enzi za ujana wake
 Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

TAKRIBANI watu 49 wamefariki dunia na wengine 48 wakijeruhiwa katika shambulio la kigaidi lililotekelezwa katika misikiti miwili ya Lin Wood na Al Noor katika mji wa Christchurch nchini New Zealand.

Waziri mkuu nchini humo Jacinda Ardern ameeleza kuwa, "Tumekumbana na shambulio ambalo hatukulitegemea leo asubuhi, na halikuwahi kutokea awali limetusikikitisha" ameeleza Jacinda.
Aidha jeshi la polisi limethibitisha kukamatwa kwa washukiwa watatu wakiwemo wanaume wawili na mwanamke mmoja na mmoja kati yao akiwa raia wa Australia huku washukiwa zaidi wakiendelea kutafutwa.

Imeelezwa kuwa mmoja kati ya washukiwa hao ni mwanaume ambaye enzi za ujana wake aliwahi kuwa na tuhuma za mauaji. Aidha polisi wamesema hali si shwari na imeamuliwa misikiti yote nchini humo kufungwa hadi amri ya kufunguliwa itakavyotolewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...