Wananchi wa jijini Mwanza wamejitokeza katika kupima afya katika maadhimisho ya Figo Duniani katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando .

Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku Figo Duniani Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. Bahati Wajanga amesema kuwa ugonjwa wa figo unasumbuliwa na magojwa yasiyoyakuambukiza ya sukari na shinikizo la damu.

Amesema kuwa tafiti zinaonyesha kwa magonywa yasiyoyakuambukiza kukua nchini na hiyo ni kutokana mfumo wa maisha ya ulaji na kutofanya mazoezi ambapo katika maadhimisho haya ni kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kufundisha suala la afya katika chuo chetu .

Amesema katika maadhimisho ya siku mbili za Machi 13 na 14 ni wananchi wajitokeze katika kupima afya zao kwani kinga ni bora kuliko tiba,Amesema kauli mbiu ya maadhimisho ni Afya ya Figo kwa kila mmoja Popote ikiwa na maana huduma za afya za Figo zinatolewa popote pale kwa mwananchi alipo.

"Bugando tumejipanga katika kutoa huduma kwa wananchi kwa magonjwa yote pamoja na kutoa elimu kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza yasiendelee kupewa nafasi kwa jamii yetu na tutaendelea kuadhimisha kila mwaka".amesema Dkt Wajanga 

Nae Daktari Bingwa Idara ya Tiba, Kitengo cha Figo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando Said Kanenda amesema kuwa ugonjwa wa figo unatibika hivyo wananchi watumie fursa ya kupima afya kila mara.

Amesema kuwa katika maadhimisho hayo ndio wakati mwafaka kupima magonjwa mbalimbali na pale wanapobainika kuanza kupata tiba kabla ya ugojwa haujawa mkubwa.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani yaliyofanyika Hospitalini hapo jijini Mwanza.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika upimaji wa afya katika maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando
Daktari Bingwa, Idara ya Tiba Kitengo cha Figo wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando Dkt Said Kanenda akitoa maelezo katika maadhimisho ya Siku ya Figo Diniani yaliyofanyika katika Hospitali hiyo ambapo katika maadhimisho hayo wananchi wamejitokeza kupima afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...