NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, imeridhishwa na mabadiliko makubwa ya kiutendaji ndani ya Shirika la Umeme Nchini TANESCO, ambapo ndani ya kipindi kifupi limeondokana na utegemezi wa ruzuku ya serikali na sasa linajiendesha lenyewe. 
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Raphael M. Chegeni wakati wa hitimisho la ziara ya Kamati kwenye mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme utokanao na gesi asilia, Kinyerezi 1 (Kinyerezi I Extension) jijini Dar es Salaam, leo Machi 18, 2019.
“TANESCO ni Shirika ambalo limekumbwa na changamoto nyingi miaka ya nyuma, lakini tumefurahi kuona kwamba baadhi ya mambo yaliyokuwa mazito sana mmefanikiwa kuyatatua na hii ni dalili njema ni nzuri sana kwa sababu sasa hata serikali yetu ya awamu ya tano toka imeingia madarakani, TANESCO badala ya kuwa mtegemezi mkuu wa ruzuku ya serikali, hivi sasa Shirika halitegemei tena ruzuku ya serikali hili ni jambo jema sana.” Alisema.
Mmetoka kwenye ruzuku na sasa mnakua mnajitegemea haya ni mafanikio endeleeni kupunguza gharama, na mpanue wigo wa watumiaji wa umeme, watanzania wanahitaji umeme wenye gharama nafuu na haya ndio malengo ya serikali ya awamu ya tano, alisema Dkt. Chegeni na kuongeza
Mpango wa Serikali wa kujenga umeme wa maji kule Rufiji ni mpango sahihi kabisa na watanzania wote wazalendo lazima tuunge mkono juhudi hizo kwa sababu tunahitaji umeme ambao ni wa gharama ya chini ili  umeme umfikie kila mtanzania kwa gharama nafuu.
Aidha Mwenyekiti huyo ameahidi kuwa Kamati yake itaiomba serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina iangalie namna gani madeni yanayoikabili TANESCO kwa miaka mingi yanaondolewa ili iweze kujiendesha kikamilifu na kwa ufanisi zaidi.
“Madeni ambayo TANESCO inadaiwa huko nyuma Serikali iyabebe.” Alisisitiza. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO, Mhandisi Dkt. Alexander Kyaruzi ameiambia Kamati hiyo kuwa Kituo cha kuzalisha umeme wa gesi asilia cha Kinyerezi I kina uwezo wa kutoa Megawati 150 kwa sasa na upanuzi  unaoendelea hivi sasa utaongeza Megawati 185 na hivyo mradi utakapokamilika mwezi Agosti mwaka huu wa 2019, Kinyerezi I na I Extension itakuwa na jumla ya Megawati 335, huku Kinyeerzi II ambayo imekamilika ina uwezo wa kuzalisha Megawati 240 za umeme.
“Kinyerezi itakuwa complex kubwa sana ya kuzalisha umeme, tutaendelea na ujenzi wa Kinyerezi III na Kinyerezi IV.” Alifafanua.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka alisema Shirika limejiwekea mikakati endelevu ili kuhakikisha linaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ambapo baada ya kudhibiti deni ambalo Shirika limekuwa likidaiwa kwa muda mrefu, sasa wameanza kuwalipa wadai wa Shirika sambamba na kuondokana na kutegemea ruzuku ya kutoka serikalini.
"Kwa takriban miezi minane iliyopita deni ambalo TANSECO tumekuwa tukidaiwa limepungua kwa asilimia 3 naweza kusema limedhibitiwa." Alisema na kuomba sasa ni vema kama Serikali ingelichukua hilo deni au kututafutia mkopo ili tulimalize deni hilo kwani hii itapunguza uwezekano wa kuongezeka kutokana na interest maana tunashindana na deni lenyewe." Alifafanua Dkt. Mwinuka.
Alisema Kwa mwaka TANESCO ilikuwa ikipatiwa ruzuku ya serikali kati ya shilingi Bilioni 449 na bilioni 6 kwa mwaka, lakini hiyo sasa ni historia kwani Shirika linajiendesha lenyewe na kwa mwaka huu wa fedha tuna...project Shirika litatengeneza faida ya Shilingi Bilioni 9 

Aidha Mkurugenzi wa Uwekezaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Lightnes Mauki amesema, kwa sasa TANESCO imeanza kulipa madeni na tangu Mwezi wa Februari mwaka huu 2019 wamelipa bilioni 38.7 na ni hatua nzuri na wamekuwa wakitupatia nakala za malipo kila mwezi wanapolipa.” Alisema Lightnes
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, ambaye piamni Mbunge wa Busega, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni (kushotoO), akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara ya Kamati yake kutembelea mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme wa gesi asilia Kinyerezi I (Kinyerezi I Extension) jijini Dar es Salaam leo Machi 18, 2019.
 Wajumbe wa Kamati hiyo wakipatiwa maelezo ya utekelezaji wa mradi huo.
  Wajumbe wa Kamati hiyo wakipatiwa maelezo ya utekelezaji wa mradi huo.
 Mjumbe w aKamati Mhe. Charles Mwijage, akizungumza.
 Mbunge wa Kasulu Vijijini Mhe.Vuma Augustine ni miongozi mwa wajumbe waliotembelea mradi huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Mhandisi Dkt. Alexander Kyaruzi (aliyesimama), akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara ya kamati Machi 18, 2019. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka akizungumza.
Dkt. Mwinuka akimkaribisha Mbunge wa Karatu, Mhe. Willy Qambalo huku Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Dkt. Kyaruzi akishuhudia, wakati wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwkwzaji wa Mitaji ya Umma (PIC).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...