*Ni baada ya mashahidi kukosa nauli ya kuwafikisha mahakamani 

Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

KWA mara nyingine tena, kesi ya kumiliki mali isiyolingana na kipato chake inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai na wenzake imekwama kuendelea kusikilizwa kwa kuwa mahakama haina fedha ya kuita mashahidi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Awamu Mbagwa amedai leo mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa wameshindwa kuita mashahidi kutoka nje ya Dar es Salaam kwa sababu hawana fedha za kuwalipia nauli.

Mbagwa amedai kesi hiyo ilipangwa leo Machi 26, 2019 kwa ajiri ya kusikilizwa shahidi wa upande wa mashtaka lakini wameshindwa kuwaita mashahidi kwa sababu hawana fedha za kuwalipia nauli. 

"Tumeshindwa kupata mashahidi kwa sababu wote wanatoka nje ya Jiji la Dar es Salaam na wamesema hawana uwezo wa kujisafirisha kuja kutoa ushahidi, " amedai Mbagwa.Wakili wa utetezi Alex Mgongolwa amedai anaomba suala la kuwaita mashahidi lifanyiwe kazi haraka.

Hata hivyo Hakimu Simba amesema, malipo ya mashahidi yana utaratibu wake na kwamba mahakama yake italifanyia kazi na watalitatua suala hilo kwani linazungumzika.Kwa kukumbusha tu ni mara ya pili kwa kesi hiyo imekwama kuendelea kusikilizwa baada ya mwanzoni mwa Oktoba mwaka jana kushindwa kusikilizwa kwa ukosefu wa fedha.

Kesi hiyo itasikilizwa Aprili 8, mwaka huu na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu. Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

Gugai na mwenzake watatu wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo, makosa 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.

Katika kesi ya msingi, Gugai na mwenzake, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.

Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decemba 2015.

Inadaiwa akiwa Takukuru Dar es Salaam, Gugai alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh.bilioni 3.6 ambazo hazilingani na kipato chake huku akishindwa kuzitolea maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...