Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Tanga Doris Wilson wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa viongozi wa ngazi mbalimbali ikiwemo mabaraza,wenyeviti na wajumbe juu ya ujuaji wa sheria na kufata taratibu na kutoa maamuzi sahihi ili kuweza kutatua migogoro ulioandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) na kufanyika mjini hapa 
Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) Latifa Ayoub akizungumza wakati wa warsha hiyo 
Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) Mwanaidi Kombo akisisitiza jambo wakati wa warsha hiyo 
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo 
Sehemu ya wajumbe wa warsha hiyo wakifuatilia 


KUKOSEKANA elimu kwa wajumbe wengi waliopo kwenye mabaraza ya ardhi na nyumba ngazi ya kata kumeelezwa kuchangia kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa waledi mkubwa na kusababisha migogoro kwa wananchi na manung’uniko.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Tanga Doris Wilson wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa viongozi wa ngazi mbalimbali ikiwemo mabaraza,wenyeviti na wajumbe juu ya ujuaji wa sheria na kufata taratibu na kutoa maamuzi sahihi ili kuweza kutatua migogoro ulioandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) na kufanyika mjini hapa.

Alisema elimu hiyo itakuwa chachu kwa wajumbe hao kuweza kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwenye mabaraza hayo lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha wanatenda haki kwa wananchi ambao wanakabiliwa na migogoro mbalimbali kwenye maeneo yao.

“Changamoto kubwa ya mabaraza ya Kata ni elimu wajumbe wengi hawajapata elimu kuhusu mabaraza hayo, muundo, namna ya utendaji, akidi katika kuendesha na utaratibu wa kuendesha mashauri hivyo tunaamini kupitia elimu hii inaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye utekelezaji wa shughuli zenu “Alisema Mwenyekiti huyo.

“Lakini pia tunaishukuru Tawla kwani wanapotoa mafunzo ya namna hii wanawapa wajumbe uelewa kuhusu namna ya kuendesha mashauri hayo,kwa kufanya hivyo haki kwa wananchi inaweza kutendeka na kuondoa manung’uniko “Alisema 

Aidha alisema mikakati waliokuwa nayo hivi sasa ni kuhakikisha wanatoa elimu kwa mabaraza ya ngazi ya kata ili waweze kufanya kazi zao kwa waledi mkubwa katika kutoa haki pindi wanapopelekewa malalamiko kutoka kwa wananchi.

Awali akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) Latifa Ayoub alisema lengo la warsha hiyo ni kutoa elimu kwa ngazi mbalimbali kwa viongozi wa mabaraza,wenyeviti na wajumbe ili waweze kujua sheria na kufuata taratibu na kutoa maamuzi sahihi wakati wakitatua migogoro.

Mratibu huyo alisema warsha hiyo imehusisha wajumbe, makatibu na wenyeviti wa mabaraza ya ardhi kutoka kwenye kata mbili za Magila na Kilulu kwalengo la kuwajengea uwezo wa kufahamu sheria za ardhi na kuto maamuzi sahihi kwa wananchi.

Hata hivyo alisema watajaribu kuangalia jinsi gani ya kuweza kushirikiana kwa pamoja kupunguza changamoto hizo yakiwemo mashauri mengi yaliwepo kwenye baraza hilo hali itakayowezesha kuondosha migogoro kwa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...