Na: Moshy Kiyungi

Aliyekuwa mtunzi na mwimbaji maarufu Lovy Longomba, aliweza kuzifuata nyayo za uimbaji wa baba yake Vicky Longomba.

Baba yake huyo alikuwa mtunzi na mwimbaji wa kutegemewa katika bendi ya T.P.OK. Jazz, iliyokuwa ikiongozwa na Luambo Makiadi Lokanga La dju Pene Francois ‘Le Grand Mitre’.

Zipo familia zilizojaaliwa kuwa vipaji vya wacheza mpira wa miguu, nyavu, ngumi, na michezo mingine.

Mfano ni fimiliya ya wanadada wawili Wamarekani weusi, Serena na Vunus Williams, ambao ni mabingwa Kimataifa katika kucheza mpira wa Tennis.

Hapa nchini familia ya akina Uvuruge ilikuwa na watoto waliokuwa na vipaji vya kutunga nyimbo na kupiga muziki. Ndugu hao Jumanne, Stamili, Huluka na Maneno, walijijengea sifa tele katika muziki hapa nchini.

Familia ya akina Katwila, wapo akina Shabani, Adam na….

Aiha familia ya akina Kihwelu nayo ilikuwa ni ya vipaji vya kucheza mpira wa miguu, ambapo walikuwepo akina Mtwa, Jamhuri ‘Julo’ na ndugu zao wengine.Kwa upande wa ngumi, familia ya Matumla imerithisha kucheza mchezo wa ndondi takribani familiya nzima.

Katika makala hii ambayo inaizungumzia Familia ya Longomba, toka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Vicky Longomba ndiye aliye kuwa baba wa familia ya watoto wengi waliojaaliwa vipaji vingi vya muziki.

Huyo Mzee Vicky Longomba alikuwa mmoja kati ya wanamuziki waliokuwa waanzilishi wa bendi ya T.P.OK. Jazz iliyokuwa ikiongozwa na Franco Luanzo Makiadi.Ikumbukwe kwamba Vicky ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa bendi ya Lovy du Zaire, iliyotamba katika muziki nchini Kongo mwaka 1971.

Kwa kuwa familia hiyo ina wanamuziki wengi leo katika makala hii nitamzungumzia mmoja wa watoto wake Lovy Longomba.Wasifu wa mwanamuziki huyo unaelezea kwamba alianza muziki katika bendi ya Orchestra Macchi mwaka 1976, akiwa na mwimbaji mwenzake Dindo Yogo.

Aidha walikishirikiana na mpiga gitaa Nseka Huit, baadaye waliondoka katika bendi ya Macchi, wakaenda kuunda bendi yao ya Etumba. Baadhi ya wanamuziki waliokuwepo kwenye kundi hilo ni waimbaji akina Lofanga, Gaby Yau-Yau na Mukolo, aliyekuwa akiimba sauti ya kwanza.

Wanamuziki wengine waliokuwepo katika bendi hiyo ni pamoja Ngwaka na Huit Kilos, ambaye baadaye alikwenda kuwa nyota katika bendi ya Afrisa International ya Tabu Ley Rochereau.

Mwanamziki Ricardo aliondoka na kwenda katika bendi ya Lemvo in Makina Loca, iliyo na makao yake huko Los Angeles, nchini Marekani.Yaelezwa kwamba Lovy Longomba alikuwa na vipaji vya utunzi, uiimbaji mahiri pamoja na unenguaji wakti mwingine.

Alikuwa kaka wa wanamuziki machachari Awilo Longomba, ambaye kabla ya kuanza kutunga na kuimba, alikuwa mcharazaji hodari wa drums katika bendi mbalimbali nchini humo.

Lovy naye pia alikuwa baba wa familiya yenye watoto wanamuziki akiwemo binti yake aliyerithi uimbaji, Elly Longomba na mapacha Christian na Lovy ambao wote ni nyota katika muziki wa Hip-hop, wakimiliki Kampuni ya ‘Longambas’ huko Nairobi, nchini Kenya.

Baadaye Agosti 1978, Lovy aliicha bendi ya Orchestra Macchi, na kuamua kuondoka Kinshasa.Alitiga katika jiji la Nairobi nchini Kenya ambako alijiunga katika bendi ya Les Kinois.

Kwa kuwa ‘Kiu’ chake hakichakidhiwa, Lovy alidumu kwa miezi mitatu pekee,akatimkia katika bendi ya Boma Liwanza.Lakini huko nako hakudumu kwa kipindi kirefu kwa kuwa baada ya miezi sita, alitimka na kuiacha Boma Liwanza.

Lovy akaenda kujiunga na bendi ya Super Mazembe iliyokuwa ikiongozwa na Mutonkole Longwa Didos.Akiwa katika bendi hiyo alionesha uhodari wa kutumia sauti yake ilivyokuwa nyembemba na nyororo, ambayo ndiyo iliyopelekea kwa yeye kupachikwa jina bandia la ‘Ya Mama’. Sababu kubwa ni kwamba alikuwa na uwezo wa kuimba sauti ya juu ambayo alipashwa aimbe wanamke.

Katika bendi Super Mazembe alikutana na wanamuziki wenzake mahiri akina Joseph Okello Songa, Kasongo wa Kanema, Musa Olokwiso Mandala na Fataki Lokassa ‘Masumbuko ya duniya’ aliyekuwa ametokea katika bendi ya Les Kinois.

Baadhi ya nyimbo alizoachia katika bendi hiyo ni pamoja na ‘Lovy’, ‘Yo Mabe’, ‘Ndeko’, ‘Nanga’, ‘Mokano’ na ‘Elena’.

Sauti yake nyororo mara nyingi husikika katika baadhi ya nyimbo za bendi hiyo, akibwagiza akitamka “Vuta sigara SM, maana yake Super Mazembe…”

Hata hivyo umahiri wa kutunga na kuimba katika bendi hiyo, ilisababisha kuhitajika takribani na kila bendi.

Kwa mara nyingine tena Lovy aliondoka Super Mazembe mwaka 1981 akaenda kuimba katika bendi ya Shika Shika, iliyokuwa ikiongoza na Jimmy Monimambo, kwa kipindi cha miaka miwili.

Ndoto zake za kumiliki bendi yake zilitimia baada ya yeye na wanamuziki wenzake alipounda bendi yake Super Lovy ikiwa na Nembo ya AIT.

Lakini kwa kile alichokieleza ni kuepuka mkanganyiko na mvutano aliamua kutumia jina Bana Likasi wakati aliporekodi katika Kampuni ya Audio Productions Ltd.

Mnamo mwaka 1988 Lovy aliingia Tanzania katika jiji la Dar es Salaam na akapigia katika bendi Orchestra Afriso Ngoma.

Maisha ya nguli huyo yalikatishwa ghafla katika ajali iliyopelekea kufariki dunia nchini Tanzania mwaka 1996.

Mungu aiweke roho yake pahala pema peponi, amina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...