Nafasi za masomo na ajira

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwahimiza Watanzania wenye sifa kuomba fursa za masomo na ajira zinazotolewa na wadau mbalimbali duniani. Fursa zilizopokelewa mwezi Machi 2019 ni kama ifuatavyo:

i.       Mafunzo ya Shahada ya Uzamili yanayotolewa na Chuo Kikuu cha British nchini Misri (British University – Egypt) kwa kipindi cha mwaka wa masomo 2019/2020. Fursa hizi zinaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, na maombi yanafanyika kwa njia ya  mtandao kupitia tovuti, http://www.bue.edu.eg/;

ii.    Mafunzo ya Shahada ya Kwanza na Uzamili yanayotolewa na Taasisi ya Elimu ya Urusi (Russian Education Institute)                                               kwa kipindi cha mwaka wa masomo 2019/2020 na 2020/2021. Fursa hizi zinaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Maelezo ya namna ya kuomba fursa hizo yanapatikana katika Wizara zinazoratibu mafunzo hayo. Mwisho wa kufanya maombi kwa mwaka wa masomo 2019/2020 ni tarehe 25 Machi 2019 na tarehe 25 Juni 2020 kwa mwaka wa masomo 2020/2021;

iii. Mafunzo ya Shahada ya Uzamili katika fani ya Usuluhisihi katika Mchakato wa kutafuta Amani (Mediation in Peace Processes) yatakayotolewa nchini Ujerumani katika kipindi cha mwaka wa masomo 2019/2021.  Fursa hizi zinaratibiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki, na maombi yanafanyika kwa njia ya mtandao kupitia tovuti, http://www.mas-mediation.ethz.ch/.  Mwisho wa kufanya maombi ni tarehe 21 Aprili 2019;

NAFASI ZA AJIRA
iv. Nafasi ya ajira ya Afisa Tathmini (Evaluation Officer, P-3) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Kudhibiti Matumizi ya Silaha za Kemikali (The Secretariat of the Organization for the Prohibition of Chemical Weapons-OPCW). Maelezo ya jinsi ya kuomba yanapatikana katika tovuti, https://opcw-career.talent-soft.com/job/job-officer-industry-p-3_11.aspx. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15 Machi 2019; na

v.    Nafasi ya ajira ya Afisa Usalama wa Masuala ya Habari (Information Security Officer, P – 3) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Kudhibiti Matumizi ya Silaha za Kemikali (The Secretariat of the Organization for the Prohibition of Chemical Weapons-OPCW). Maelezo ya jinsi ya kuomba yanapatikana katika tovuti, https://opcw-career.talent-soft.com/job/job-information- security-officer-industry-p-3_18.aspx. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 26 Machi 2019.
         

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
13 Machi 2019

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...