Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amewataka watumishi waliopo katika wizara hiyo kubadilika na kuboresha utendaji kazi na kutekeleza majukumu yao kwa weledi,kasi na uzalendo usiotiliwa mashaka sema wizara usiotiliwa mashaka kwa kuwa Wizara hiyo ndio kioo cha Taifa.

Akizungumza katika kikao kilichowakutanisha watumishi wote wa wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki uliofanyika Dodoma kwa mara ya kwanza tangu ateuliwa kuiongoza wizara hiyo,Profesa Kabudi amesema ilani ya chama cha mapinduzi imetoa maelekezo yanayopaswa kutekelezwa na wizara hiyo ikiwa ni pamoja na kusimamia uchumi wa viwanda pamoja na diplomasia ya kiuchumi.

“Ilani ya Chama Cha Mapinduzi imetoa mambo ambayo yanapaswa kutekelezwa na Wiazara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki ambayo yako wazi kabisa ikiwa ni pamoja na kusimamia uchumi wa viwanda pamoja na diplomasia ya uchumi ambayo itaisaidia Tanzania kujenga uchumi imara utakaowezesha kutoa huduma za kijamii na kutoa ustawi kwa watanzania wote”

Ameongeza kuwa ili lengo hilo litimie ni lazima sasa watumishi wote wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kufanya kazi kitimu kwa kushirikiana na wizara nyingine kwa Mslahi mapana ya Taifa.

Amesema kuwa wizara hiyo ni nyeti kwa kuwa ndio sikio,jicho na msemaji wa nchi kimataifa hivyo watumishi hawana budi kujituma na kuongeza kasi na weledi ili kufikia malengoya wizara hiyo na matarajio ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Aidha Profesa Palamagamba John Kabudi mbali na kuwataka watumishi wa wizara hiyo kutekeleza masuala yaliyoahidiwa kupitia ilani ya chama cha mapinduzi,amewataka pia kuzingatia hotuba iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akilizindua Bunge 11, Novemba 20,2015.

Amesema amelazimika kukukutana na watumishi wa wizara hiyo kwa kuwa imekuwa na taswira ambayo haijafikia matarajio yanayotarajiwa na ili iweze kufikia malengo hayo ni budi kuzingatia maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na Hotuba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ya uzinduzi wa Bunge la 11 kwa kuwa wizara hiyo italazimika kutoa mrejesho wa kile kilichotekelezwa kupitia maagizo hayo ya Ilani na Hotuba ya Rais.

Amewataka pia watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki wawe tayari kubadilika na kufanya kazi mahali popote kwa kuwa lengo la serikali ya awamu ya Tano na vipaumbele vyake inaweza kumuhitaji mtumishi yeyote wa uma kwenda kufanya kazi popote kulingana na mahitaji.“Ni imani yangu kuwa wtumishi wa wizara hii wamenielewa na sasa watatekeleza majukumu yao kwa kasi,weledi,uelewa na uaminifu usiotiliwa mashaka ili kufikia matarajio ya watanzania katika wizara hii”
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa wizara yake, wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Faraji Kasidi Mnyepe, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi (wa pili kutoka kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu Bi. Severa Kazaura (wa kwanza kushoto) na wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi Wizarani (TUGHE) Bw. Hassan Mwinyi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Pro. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Joachim Otaru. Tukio hilo limefanyiaka wakati Profesa Kabudi alipokutana na Kufanya Mkutano na Wafanyakazi wa Wizara yake ikiwa ni kwa mara ya kwanza tokea ameteuliwa na Rais wa Ja,huri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Katikati ni Katibu mkuu wa wizara hiyo Dkt Faraji Kasidi Mnyepe akishuhudia tukio hilo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Wizara yake pamoja na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, mara baada ya kumaliza mkutano kati ya Profesa Palamagamba John Kabudi na Watumishi wote. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...