Na Ndimmyake Mwakapiso
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. John Mongela, imefanya ziara rasmi katika ukumbi wa BOT kukagua maandalizi ya kikao kazi cha Maofisa Mawasilino Serikali kinachotarajiwa kufungulia na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa, Jijini humo.

Akitoa tathmini yake mara baada ya ukaguzi wa ukumbi wa mkutano huo, Mkuu wa Mkoa ameridhishwa na mandalizi yanayoratibiwa kwa pamoja na Idara ya Habari MAELEZO kwa kushirikiana na Uongozi wa Chama cha Maofisa Mawasiliano Serikalini TAGCO.

“Mnakwenda vizuri, naona kila kitu kipo vizuri na kwa maandalizi haya ni imani yangu kuwa mkutano huu utaenda vizuri na msisite kutufahamisha endapo kutakuwa na mabadiliko yoyote”.

Mapokezi ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, yaliongozwa na Mkurugenzi wa idara ya Habari Maelezo ambaye pia ndiye msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abasi na viongozi wa chama cha Maofisa Mawasiliano Serikalini TAGCO.

Kikao hicho ni cha siku tano kinachotarajiwa kuanza siku ya Jumatatu, Machi 18 hadi Ijumaa 22, mwaka huu kinachotarajiwa kuwakutanisha zaidi ya Maofisa Mawasiliano 300 kutoka Wizara, Mashirika ya Umma, Taasisi za Serikali, Tawala za mikoa na Serikali za mitaa.
Mkuu wa Mkoa huo Mhe. John Mongela,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...