Anaandika Abdullatif Yunus, 
Michuzi Blog, Bukoba - Kagera.

Maadhimisho ya siku ya  Muungano wa utepe mweupe na uzazi salama  katika Mkoa wa Kagera yamefanyika Kitaifa Mkoani Kagera Machi 15, 2019 huku  jamii ikihimizwa kuacha ukatiri wa kijinsia kwa wanawake na wasichana.
Awali Maadhimisho hayo yalitanguliwa na mandamano ya wananchi mamia kwa maelfu na kisha kilele chake Kufanyika katika viwanja ya Gymkana katika manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera  yakiwa na kauli mbiu "komesha  unyanyasaji kwa wanawake na wasichana,okoa maisha wakati wa uzazi".



Meneja Mawasiliano kutoka  muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama Anna Sawaki amesema maadhimisho hayo kuwa yana lengo la kupunguza vifo kwa wananwake wakati wa kujifungua. Na kuongeza
kuwa takwimu zinaonesha vifo vitokanavyo na uzazi vinaongezeka badala ya kupungua kutokana na unyanyasaji wanaoupata akina mama pindi wawapo wajawazito na wakati wa kujifungua.



Kwaupande wake Rose Mlayi  ambaye ni mratibu wa Taifa wa muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama ameiomba jamii  kukomesha ukatili kwa wanawake na wasichana, ili kuokoa maisha yao wakati wa uzazi.
Bi Rose amesema kuwa upungufu wa vituo vya afya na zahanati katika maeneo mengi ni moja ya vyanzo vinavyosababisha vifo kwa akina mama wengi wakati wa kuelekea kujifungua hasa maeneo ya vijijini kutokana na wamama hao kutembea mwendo mrefu pamoja na baadhi ya mira potofu kutoka kwa jamii ya kuwazuia wanawake kujifungulia katika vituo vya afya.



Katika hotuba ya Waziri wa afya,maeneleo ya jamii jinsia wazee  na watoto Ummy Mwalimu iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo,amesisitiza kuwa Serikali kupitia idara zake inaendelea kukomesha vitendo hivyo, ikiwemo kuendelea na mikakati yake ya kutokomeza vifo vitakavya na uzazi pingamizi.
Waziri ummy ameongeza kuwa wizara yake inaendelea kuboresha sekta ya afya hasa upande wa vituo vya afya pamoja na vifaa tiba ambapo pia ameeleza mkakati wa kuanzisha vituo vya huduma jumuishi kwa kila kituo cha afya.

 Meneja mahusiano kutoka shirika la utepe mweupe Anna kushoto akitoa maelezo juu ya kazi wanazozifanya katika kupambana na vifo vitokanavyo na uazazi
Mgeni rasmi Deodatus Kinawiro kwa Niaba ya Waziri Ummy Mwalimu akizindua mpango wa utepe mweupe katika maadhimisho yaliyofanyika Manispaa ya Bukoba 
 Mgeni rasmi Deodatus Kinawiro Mkuu wa Wikaya ya Bukoba akionesha mpango wa utepe mweupe Mara baada ya kuzindua 
 waandamanaji na wadau wa sekta ya Afya, wakitembea kwa maandamano wakikatiza maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Bukoba kuelekea viwanja vya Gymkhana.
Waendesha bodaboda na wadau wa sekta ya Afya, wakiwa katika maandamano maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Bukoba kuelekea viwanja vya Gymkhana.
Waandamanaji na wadau wa sekta ya Afya, wakitembea kwa maandamano wakikatiza maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Bukoba kuelekea viwanja vya Gymkhana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...