Waajiri katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekretarieti za mikoa wametakiwa kutoa mafunzo kwa wajumbe na viongozi wapya wa mabaraza ya wafanyakazi ili waweze kumudu majukumu yao ya kusimamia haki za watumishi ipasavyo.

Rai hiyo  imetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi la ofisi yake kilichofanyika katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.

Dkt. Michael amesema kuwa, endapo waajiri wataweka utaratibu wa kutoa mafunzo kwa viongozi na wajumbe wa mabaraza mapya ya wafanyakazi, itawawezesha kufahamu majukumu yao vizuri.
“Wajumbe wa mabaraza ya wafanyakazi wakiingia kwenye mabaraza bila kujua majukumu na wajibu wao hawatawatendea haki wafanyakazi waliowachagua na kuwaamini kuwawakilisha kwenye mabaraza hayo” Dkt. Michael amesema.

Dkt. Michael ameongeza kuwa, mafunzo kwa viongozi na wajumbe wa mabaraza ya wafanyakazi serikalini yatasaidia kuondoa hali ya ufanyaji kazi kwa mazoea. Dkt. Michael amefafanua kuwa, lengo la kuwapo kwa mabaraza ya wafanyakazi serikalini ni kujadili hoja za watumishi kupitia wawakilishi katika mabaraza ya wafanyakazi ili kuwapo na maslahi mazuri na pia kuongeza tija katika utendaji kazi wa wafanyakazi.

Naye, Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Lilian Denis amewataka wawakilishi wa watumishi katika mabaraza ya wafanyakazi kuhakikisha wanawasilisha masuala ya msingi katika mabaraza hayo ili kupatiwa ufumbuzi ambao utaongeza ari ya utendaji kazi ndani ya taasisi husika.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Menyiaichi Koka amesema kuwa uwapo wa mabaraza ya wafanyakazi serikalini utasaidia kuongeza nidhamu ya kazi, kukuza maadili ya utendaji kazi na kuepusha migogoro sehemu za kazi.
Baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora limehudhuriwa na  wajumbe wa baraza hilo, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na wawakilishi wa TUGHE tawi la Utumishi ambao wamepata fursa ya kujadili mambo yanayohusu ustawi wa watumishi, motisha za watumishi, vitendea kazi, mazingira bora ya kufanya kazi na namna bora ya kuimarisha mahusiano mazuri kazini.
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael  akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi la ofisi yake (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Lilian Denis.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael  akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi la ofisi yake katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael (hayupo pichani) katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael  akikabidhi moja ya hati ya kiwanja kwa mtumishi wa ofisi yake,Bw. Jumbe Mgoha wakati wa kikao cha baraza  la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph.
 Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael (kulia) akikabidhi moja ya hati ya kiwanja kwa mtumishi wa ofisi yake, Anna Zahoro  wakati wa kikao cha baraza  la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael (wa pili kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora baada ya kikao cha baraza la wafanyakazi la ofisi yake  kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...