Na Woinde Shizza,Arusha

Naibu waziri wa kilimo Mh Inocent Bashungwa amewaagiza watafiti wa kilimo kuhakikisha wanatafsiri matokeo ya tafiti kwa lugha ya kiswahili ili iweze kueleweka kwa wakulima, badala ya kutumia lugha ya kiigireza ambayo mwisho wa siku haiwanufaishi wakulima.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika uzinduzi wa teknolojia ya kilimo hifadhi ijulikanayo kwa jina la CASI iliyofanyika mjini hapa.

Alisema kuwa,tafiti nyingi ambazo zimekuwa zikifanyika zimekuwa zikiandaliwa kwa lugha ya kiingireza hali ambayo imeshindwa kuwafikia walengwa wengi ambao ni wakulima ,hivyo lazima pawepo na mabadiliko hayo ili ziwafikie walengwa kwa wakati.

Alisema kuwa,teknolojia hiyo inajikita katika kuleta mabadiliko makubwa kwa wakulima hususani katika kuongeza uzalishaji zaidi kutokana na teknolojia hiyo kustahimili ukame kwa kiwango kikubwa.

Kwa upande wake mkuu wa mradi wa SIMLESA ,Dkt John Sariah amesema kuwa,mradi huo umewafikia zaidi ya wakulima elfu hamsini ,ambao wamefikiwa moja kwa moja huku zaidi ya wakulima zaidi ya elfu kumi na tano wakiwa wamepata taarifa juu ya mradi huo.

Alisema kuwa ,mradi huo ulianza kufanya kazi mwaka 2010 ambapo walifanya tafiti katika katika wilaya mbalimbali na kugundua manufaa ya mradi huo kwani unafanya kazi katika maeneo yote hasa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi huku ukiokoa muda wa mkulima kwa asilimia 50.

Nae Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania TARI ,dokta Geoffrey Mkamilo,amesema kuwa,utafiti unaonyesho kuwa teknolojia hiyo ina manufaa makubwa kwa wakulima na tayari imeshaonyesha matunda kwa baadhi ya wakulima ambao wameshaitumia teknolojia hiyo .

Dokta Mkamilo amesema kuwa,watahakikisha teknolojia hiyo inawafikia wakulima wote ili waweze kunufaika na kuongeza uzalishaji zaidi ,ambapo watahakikisha wanaingiza utaratibu wa kuhaulisha teknolojia hiyo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa utafiti kituo cha selian ambao ndio walioibua teknolojia ya kilimo hifadhi dokta Joseph Ndunguru amesema wanahitaji teknolojia hiyo iwafikie wakulima wengi ili iweze kuongeza uzalishaji wa chakula ,hata kuongeza malighafi kwenye viwanda.

Bi Rehema hasan ni mkulima kutokea mviwata morogoro ambao ni mmoja wa walionufaika na mradi huo amesema baada ya simlesa kuwapelekea mradi huo wamenufaika kwa kiwango kikubwa cha uzalishaji wa mazao kufuatia elimu waliyopatiwa.
 Naibu waziri Wa Kilimo Innocent Bashugwa  akizungumza na waandishi Wa habari mara baada ya kuzindua rasmi teknologia ya Kilimo hifadhi .
 Katibu tawala  Mkoa wa Morogoro Clifford Tandari akizungumza namna wananchi wa mkoa wake walivyoelimishwa wakati wa utafiti huo
 Mwenyekiti Wa kamati ya kudumu ya  Bunge Kilimo ,mifugo na maji Mohammed mkiwa akito ufafanuzi wa jambo katika katika uzinduzi huo 
 Mkurugenzi wa kituo cha utafiti seliani Josephy Ndunguru akizungumza na  waandishi kuhusu mipango yao mbalimbali baada ya uzinduzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...