NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE 

WATU nane wapata majeraha baada ya gari la abiria , mali ya kampuni ya Friends ikitokea Dar es salaam kuelekea Kampala nchini Uganda kupata ajali ,eneo la Kwazoka, kata ya Vigwaza, Chalinze mkoani Pwani. 

Aidha dereva wa gari hilo lenye namba za usajili, UAY 458 F aina ya Scania ,Bashiru Telu mkazi wa nchini Uganda amekimbia baada ya kutokea ajali hiyo. 

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, ACP Wankyo Nyigesa, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo mchana march 18,mwaka huu na kusema gari hiyo ilikuwa na abiria 42.

Alieleza, gari hiyo iliacha njia na kupinduka na kusababisha majeruhi hao ambapo chanzo cha ajali ni dereva huyo kujaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari. 

Wankyo aliwataja waliopata majeraha kuwa ni Kubo Zuberi (24) aliyepata jeraha katika mkono wa kulia mkazi wa Uganda ,Rudigo Benjamin (24) na Aisha Salin (34) mkazi wa Dar es salaam ameumia kichwa.

Wengine ni Theonestina Gedioni (29) mkazi wa Tabata ,Baiga Jacquie (30) mkazi wa Uganda, Nasra Amani (12) mkazi wa Dar es salaam, Farouqs Natkunda (22)mkazi wa Uganda na Hassan Omary mkazi wa Mbezi Dar es salaam. 

"Majeruhi hao walikimbizwa katika kituo cha afya Mlandizi, ambapo wanaendelea na matibabu "alifafanua Wankyo. 

Kamanda huyo alitoa rai kwa madereva wa vyombo vya moto kutii sheria za usalama barabarani. 

Vile vile wasafiri wanaotumia vyombo hivyo kuendelea kuwafichua madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani ili waweze kuchukuliwa hatua kwa kupiga namba za makamanda wa mkoa wa wakuu wa usalama barabarani.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani, ACP Wankyo Nyigesa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...