*Yaahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwa njia ya kidigitali, wagusia changamoto ya mikopo
 
Na Agnes Francis ,Globu ya jamii

BENKI ya UBA imesema inajivunia uwepo wake wa miaka 10 nchini kwani imekuwa ikishiriki kikamilifu katika kuchangia maendeleo ya nchi ya Tanzania huku ikieleza wazi moja ya changamoto kubwa iliyopo katika taasisi za kibenki ni urejeshwaji wa mikopo iliyokopwa na wateja.

Kuhusu mikakati yao katika kujiimarisha kutoa huduma kwa Watanzania katika sekta hiyo ya kibenki, imesema imeweka nguvu zaidi kutoa kutoa huduma kwa njia ya mtandao(Kidigiali) hasa kwa kuzingatia kuna idadi kubwa ya watumiaji wa simu, hivyo imetoa siri benki hiyo iko mbioni wateja watatumia WhatsApp kwa ajili ya kufanya miamala mbalimbali ya kifedha kwa maana ya kutuma au kupokea tena kwa usalama zaidi.

Wakizungumza leo Aprili 18,2019 jijini Dar es Salaam na wahariri pamoja na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, viongozi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Usman Isiaka wamesema wanajivunia kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha uchumi unaimarika na kubwa ambalo linawapa faraja ni namna ambavyo benki yao imekuwa mstari wa mbele kusaidia miradi ya maendeleo na hivi karibuni wameungana na Benki ya CRDB kutoa fedha ili kusaidia ujenzi wa mradi wa umeme wa Rufiji.

Mkurugenzi Mkuu wa United Bank For Afrika(UBA) nchini Tanzania Usman Isiaka amesema benki yao imetimiza miaka 10 tangu ifungue tawi lake nchini Tanzania na imefikisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwake ambapo ina matawi katika nchi mbalimbali Afrika na nje ya Afrika na lengo kuu la uwepo wake ni kusaidia katika kukuza uchumi na maendeleo ya nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.

"Tumekuwa tukishiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo na hii imetupa nafasi ya benki yetu kuwa mstari wa mbele kutoa fedha kwa ajili ya kuwa sehemu ya kufanikisha miradi ya maendeleo.Uwepo wetu wa miaka 10 nchini Tanzania tumekuwa tukichangia ukuaji wa uchumi kwa kutoa mikopo kwa wananchi wa kada mbalimbali,"amesema na kuongeza wataendelea kutoa kila aina ya ushirikiano kwa Serikali ili iweze kutimiza malengo yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Hata hivyo, amesema benki hiyo imeweka mkakati wa kuendelea kuwa karibu na wananchi ikiwa pamoja na kujitangaza ili ifahamike zaidi na kuongeza kwa kipindi cha miaka miwili sasa wamefanikiwa kujitambulisha na huduma za kibenki ambazo wanazitoa huku akisisitiza wameamua kujikita katika kutoa huduma kidigitali zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Corporate Mussa Kitambi ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa pamoja na mafanikio ambayo benki hiyo imeyapata kwa kutoa huduma bora kwa wateja wao, changamoto kubwa inayowakabili ni urejeshwaji wa mikopo kutoka kwa wateja wao na kwamba kwa mazingira ya sasa hata walioweka hati ya nyumba kama dhamana ya mkopo nako hakuko sawa kwani bei ya nyumba imeshuka.

"Changamoto ambayo tunakabiliana nayo ni katika eneo hili la mikopo, wapo ambao wamekopa lakini katika kurejesha kuna shida, wapo ambao waliweka hati ya nyumba lakini nako soko la bei ya nyumba limeporomoka, hivyo inakuwa ngumu fedha iliyokopwa kurejea yote.

"Pia changamoto nyingine iliyokuwa inatukabili ni katika eneo la kubadilisha fedha ambako benki zilikuwa katika wakati mgumu kwani hakukua na uhakika wa bei ya kubadilisha fedha lakini baada ya BoT kuamua kuweka mfumo mzuri sasa mambo yanakwenda vizuri.Hiyo changamoto iliyotokana na kubadilisha fedha za kigeni haiko tena,"amesema.

"Tunafahamu kuwa Serikali iliamua fedha zake zote ziwekwe Benki Kuu, hivyo baada ya kuondolewa kwa fedha hizo ilileta changamoto kwetu, hivyo baada ya kuziondoa ndio maana mtaona hivi sasa benki zote zimekimbilia kwa wananchi kwa kuwa karibu nao na kuwahudumia,"amesema Kitambi.

Ameongeza changamoto nyingine ambayo wamekuwa nayo ni kwamba walikuwa wanafanya kazi kwa sehemu kubwa na Serikali na hasa ya kuweka fedha katika benki binafsi la kwetu ni eneo hili la urejeshwaji wa mikopo kutoka kwa wateja wetu ambao tuliwakopesha.Wapo walioweka hati za nyumba lakini ukweli hivi sasa soko la nyuma liko chini.Hivyo hata unapotaka kuuza nyumba kurejesha mkopo bado haitishi.Changamoto nyingine ilikuwa ni kupanda kwa Dola lakini tunaishukuru Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kwa kuwema mfumo rasmi wa kubadilisha fedha za kigeni.

"Kabla ya BoT kutoa maelekezo katika eneo hili la kubadilisha fedha za kigeni benki yetu na huenda hata benki nyingine zilikuwa katika wakati mgumu lakini sasa kuna unafuu maana kuna mfumo mzuri katika kubadili fedha za kigeni.Kwa sasa mambo yanakwenda vizuri,"amesema Kitambi. 

Aidha Mkuu wa Kitengo cha kuhudumia Serikali na mashirika ya Umma Dominick Thimoth amefafanua wamekuwa wakisaidia kwa kutoa mikopo kwa Serikali kwenye miradi pamoja na kuchangia bajeti ya Serikali.Wakati huo huo Mkuu wa Kitengo cha Wateja UBA Asupya Nalingigwa ametumia nafasi hiyo ya kuzungumza na wahariri kuelekeza namna ambavyo wamejipanga kutoa huduma kimtandao kwa kutumia simu za mkononi na hivi karibuni watazindua huduma ya Whtsap kwa ajili ya wateja kufanya miala.
 Pia amesema katika kurahisisha namna ya kujiunga na benki yao, wanayo huduma ya mwananchi kufungua akaunti kwa kutumia simu ya mkononi kwa kusaidia huduma ya Leo ambayo ni ya kisasa.
 Mkurugenzi wa UBA Usman Isiaka akizungumza na waandishi wa habari akifafanua huduma zinazotolewa na banki ya UBA kwa serikali na hata sekta binafsi leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu Kitengo cha wateja  UBA Asupya Nalingigwa akielezea namna ya kufungua akaunti ya benki hiyo kwa kutumia mfumo wa kisasa kupitia simu kwa lengo la kutaka kuwafikia watanzania wengi leo Jijini Dar es Salaam.
 Viongozi wa Benki ya UBA wawakisikiliza maswali ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam
Viongozi wa UBA katika picha ya pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali leo Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...