Timu ya mpira wa miguu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeendelea kuonyesha ubabe kwa timu mbalimbali zinazoshiriki michezo ya Pasaka inayofanyika Zanzibar baada ya kuichapa timu ya Mwera Fc goli 1-0 katika Viwanja vya Mbweni.

Tangu kipindi cha kwanza timu hizo zimeonyesha kandanda safi huku zikishambuliana kwa zamu lakini hadi zinakwenda mapumziko hakuna timu iliyokuwa imeona goli la mwenzake. 

Aidha, mara baada kipenga kupulizwa kipindi cha pili timu ya Muhimbili ilianza kwa kasi hivyo kupata goli la mapema dakika ya 51 kupitia kwa kiungo hatari Emmanuel Teophil.

Ushindi huo umeshuhudiwa na Mkurugenzi wa Kinga, Zanzibar Dkt.Fadhili Mohamed na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dkt. Praxeda Ogweyo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Naye kocha wa timu ya Muhumibili  Teophil Joseph amesema mchezo ulikuwa mgumu na kwamba ushindi umepatikana kutokana na  maelekezo ya kocha. 

“Tunashukuru tumeshinda mechi japo kipindi cha kwanza kulikuwa na makosa madogo madogo hivyo kipindi cha pili tumerekebisha makosa hayo na kuweza kupata ushindi," amesema kocha Teophil.
 Mkurugenzi wa kinga Dkt. Fadhili Mohamedi akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya kuanza kwa mchezo huo katika uwanja wa Mbweni,Zanzibar.
 Baadhi ya washabiki na wachezaji wa timu ya Muhimbili wakifuatilia mtanange huo kwa makini.
Mchezaji wa  timu ya muhimbili, Emmanuel Teophil akifunga goli la kwanza dhidi ya Mwera Fc  ya Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...