Akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Mahakama ya ndizi Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi amesema CCM inatoa muda wa mwezi mmoja kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo kushughulika na changamoto za wafanyabiashara wa soko la Mahakama ya ndizi.

Ndg. Polepole ameyasema haya baada ya kupokea Malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wa soko hilo ya kukosekana kwa miundombinu rafiki katika soko, uchakavu wa vibanda vya kufanyia biashara, vyoo vichache, dhulma kutoka kwa baadhi ya madalali na vitisho kutoka kwa wamiliki wa kiwanda cha urafiki.

Ndg. Mkurugenzi tengenezeni mpango kazi hapa ni aibu soko la mahakama ya ndizi kuwa hivi, mnaweza kuwa na mabanda mazuri hapa, miundombinu mizuri hapa na wafanyabiashara wapo tayari kuchangia serikali vizuri bila matatizo yoyote” Ndg. Polepole

Aidha Ndg. Polepole amewahakikishia wafanyabiashara katika soko la Mahakama ya ndizi kuwa changamoto zingine za vifungashio, tuhuma za rushwa kwenye mizani ya uloye, tanangozi na kibaha na mabadiliko katika matumizi ya ardhi katika soko hilo Chama kimepokea, kitazingatia na kuleta majibu ndani ya mwezi mmoja.

Huu ni muendelezo wa ziara za kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...