Na Khadija Seif,Globu ya jamii

KAMPUNI ya kimataifa ya kibiashara ya kuuza na kununua fedha kwenye masoko kimtandao (CITL)imeamua kuzindua mafunzo ya mfumo mpya wa kibiashara kwa lengo la kuhakikisha inawasaidia vijana kutambua ni jinsi gani wataweza kujikwamua kiuchumi kupitia biashara hiyo.

Akizungumzia mafunzo hayo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha fedha kimtandao wa kampuni hiyo Christopher Shayo amesema mafunzo hayo yataendeshwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo la kuwafikia watu wengi zaidi ili kufikisha elimu hiyo.

Shayo amefafanua mafunzo hayo yanatarajia kuanza rasmi Aprili 17,2019 na kutarajiwa kuwa na wanafunzi wapatao 100 ambao watajisajiri mapema.

Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo Jimmy James amesema mafunzo hayo yatakavowafikia watu wa mikoani pamoja na nchi zingine kupitia kwenye tovuti za kampuni ya CITL na badae kuwafikia wanafunzi hao na kuendesha mafunzo kikamilifu .

" Fursa hii ni ya kipekee kwani tumefanya tafiti na kugundua asilimia kubwa ya watu bado hawana uelewa kuhusu biashara ya kuuza na kununua fedha kupitia mtandaoni," amesema James.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...