Na Hussein Stambuli-Morogoro.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Bashiru Ally amesema ili Taifa lifikie malengo ya maendeleo na amani idumu inapaswa viongozi waliopewa nyadhfa mbalimbali katika jamii kutenda haki na usawa na kuachana na wizi wa mali za umma, unyonyaji kwa wanyonge, rushwa pamoja na ufisadi.

Dk.Bashiru ameyasema hayo leo Aprili 12, 2019, wakati akizungumza na wakulima kwenye mdahalo ulioandaliwa na Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) ikiwa ni maadhimisho ya kutafakari maisha ya Waziri Mkuu wa zamani nchini Hayati Edward Moringe Sokoine kwa kuangalia mtazamo wake kuhusu maendeleo vijijini na mchango wa wakulima wadogo katika ujenzi wa uchumi wa kitaifa ambapo akataka kiongozi huyo kuenziwa kivitendo.

"Usawa ni kila binadaam anastahili heshima ya kuheshimiwa na kuthaminiwa utu wake sio usawa wa rangi wala kimo au umaarufu au uduni wao lakini woote ni binaadam ambao utu wao unastahili kuheshimiwa, na mtu anaeamini katika usawa wa binaadam lazma pia akubali katika jamii ile ile watokee watu ambao wanakula na kusaza na kutupa wakati wengine wanakufa na njaa,"amesema Dk.Bashiru.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kavazi la Mwalimu Julias Nyerere, Profesa Issa Shivji amesema wananchi hawawezi kujikomboa bila mapambano, hivyo ni muhimu kuwa na umoja na kukemea uovu wowote unaofanywa kwa kwenda kinyume na sharia na taratibu za nchi. "Lazima tuwe na chombo chetu kama wakulima chombo cha kutuelimisha, kutulinda hasa wananchi wa vijijini jambo litakalowasaidia kufahamu haki zao,"amesema Shivji.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa MVIWATA Steve Ruvuga amesema lengo kuu la mdahalo huo ni kujadili na kufikisha maoni kwenye ngazi mbalimbali ili uzalishaji uwe na tija zaidi kwa wakulima nchini."Naamini tunayoyazungumzia hapa yanahusu masuala mapana ya kilimo yanayohusu masuala mapana ya kilimo pamoja nauzalishaji wa kilimo chenyewe hasa kwa wakulima wadogo kwahiyo tunaamini tafakari ya leo itatufanya tufaham namna bora ya uzalishaji na kukuza uzalishaji."
Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (ccm) taifa dr bashiru ally akizungumza na wakulima wadogo katika maadhimisho ya kutafakari maisha ya waziri mkuu wa zamani wa tanzania  hayati edward moringe sokoine
 2. wakulima waliojitokeza katika  mdahalo ulioandaliwa na  mtandao wa vikundi vya wakulima tanzania mviwata ikiwa ni maadhimisho ya kutafakari maisha ya waziri mkuu wa zamani wa tanzania  hayati edward moringe so
 Mwenyekiti wa kavazi la mwalimu julias kambarage nyerere prof issa shivji akizungumza na wakulima wadogo katika maadhimisho ya kutafakari maisha ya waziri mkuu wa zamani wa tanzania  hayati edward moringe so
 5.katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (ccm) taifa dr bashiru ally katikati, kulia Mwenyekiti wa kavazi la mwalimu julias kambarage nyerere prof issa shivji na kuliadk.ng’wanza kamata, mhadhiri kutoka chuo kikuu ch
 Mkurugenzi mtendaji wa mviwata steven ruvuga akifafanua jambo katika mdahalo ulioandaliwa na  mtandao wa vikundi vya wakulima tanzania mviwata ikiwa ni maadhimisho ya kutafakari maisha ya waziri mkuu wa zamani .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...