Na Hussein Stambuli, Morogoro

Ubalozi wa marekani umewaapisha wafanyakazi wa kujitolea wapatao 59 raia wa marekani watakao hudumu nchini ndani ya wilaya 35 kwa muda wa miaka 2 katika sekta ya kilimo na afya lengo kuongeza uzoefu na maarifa mapya katika sekta hizo…

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kuwaapisha wafanyakazi hao kutoka shirika la wafanyakazi wa kujitolea wa kimarekani peace corps kaimu balozi wa marekani dk inmi patterson amesema kuwa wafanyakazi hao wataongeza uzoefu na maarifa katika sekta ya kilimo hasa kwa wakulima wadogo huku katika upande wa afya wakiwa na lengo la kujenga uelewa juu ya ugonjwa wa hiv na utapiamlo.

“Kupitia program hii mtaweza kuleta mabadiliko kwa watanzania mtakaofanya nao kazi na hata kwenu nyinyi wenyewe” amesema dr inmi patterson

Naibu waziri ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) mwita mwikabe amesisiti viongozi wa wilaya walizopangiwa wafanyakazi hao wameombwa kudumisha ushirikiano na wafanyakazi hao ili kuhakikisha maarifa waliyonayo wanayapokea pamoja na kulitangaza taifa katika nyanja mbalimbali na kutaka kuenziwa kwa ushirikiano huo wa kupokea wafanyakazi wa kujitolea ulioasisiwa na rais wa taifa hilo john f kennedy mwaka 1961.

“ningeomba kuweza kuwasisitiza wakuu wa wilaya na viongozi wote watakao husika moja kwa moaja kuwapokea wageni hawa ni muhimu kuwapa ushirikiano kwani kubadilishana maarifa kutasaidia wananchi wetu kujifunza mambo mapya ambayo yatasaidia kukua katika sekta ya kilimo na afya na umoja huu ni muhimu ukaenziwa” amesema mwikabe, Naibu waziri ofisi ya rais (tamisemi)

Wafanyakazi kutoka marekani waliopata mafunzo ya lugha na tamaduni kwa muda wa wiki 10 wameonesha kuvutiwa na aina ya maisha ya watanzania na wakiahidi kutoa ushirikiano zaidi kwani wanaamini watanzania wengi wanapenda kujifunza na wao watajitahidi kurithisha maarifa waliyonayo hasa kwenye sekta ya kilimo na afya bora.

“Tumefurahishwa na uwepo wetu hapa katika nchi hii tunahakika ushirikiano uliopo utatuwezesha kubadilishana uzoefu wa kiufundi na tamaduni tunauhakika tumeishi vyema na kutambua changamoto ambazo zinatukabili tumejipanga katika uvumilivu na tunaamini mwishoni wote tutafurahi kuyaona mafanikio” amesema sidney cech, muwakilishi wafanyakazi

Peace corps ni taasisi ya seriakli ya marekani iliyoanzishwa mwaka 1961 chini ya rais john f kennedy ambayo mpaka hivi sasa wafanyakazi wapatao 7000 wanahudumu katika nchi 70 duniani kwa zaidi ya miaka 50 huku lengo likiwa ni kuendesha shughuli za mabadilishano ya kiufundi na tamaduni.
 Kaimu Balozi wa Marekani Dkt Inmi Patterson akiwaapisha wafanyakazi wa kujitolea wapatao 59 raia wa Marekani watakao hudumu nchini ndani ya wilaya 35 kwa muda wa miaka 2 katika sekta ya kilimo na afya.
Kaimu Balozi wa Marekani Dkt Inmi Patterson akizungumza jambo na wafanyakazi wa kujitolea wapatao 59 raia wa Marekani.
 Wafanyakazi wa kujitolea wapatao 59 raia wa Marekani watakao hudumu nchini ndani ya wilaya 35 kwa muda wa miaka 2.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...