Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

SERIKALI imesema miradi inayoendelea hivi sasa nchini si kikwazo kinachosababisha mishahara ya watumishi kutopanda.

Pia imesema tayari bodi ya watumishi imeshafanya tafiti zake za kuangalia  viwango vya mishahara kwa kila mtumishi na kuondoa utofauti uliopo kwa baada ya kupanda kila mtumishi atafufurahi.

Imesema kinachosubiriwa hivi sasa ni vikao vya pamoja kwa ajili yakujadili kuhusiana na ripoti hiyo na baadae iweze kupelekwa kwa Rais ili iweze kufanyiwa utekelezaji.Hayo yalisemwa jana na Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Menegimenti ya Utumishi wa Umma Dkt.Francis Michael katika mkutano wa 25 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA lililofanyika Mjini Bagamoyo mkoani Pwani.

Amesema Serikali ina lengo zuri la kutekeleza miradi ya maebdeleo ambayo inatija kubwa katika Taifa.Michael amesema miradi hiyo inatekelezwa na fedha za watanzania na miradi hiyo ni faida kwa watanzania ambao fedha zao zinatumika hivi sasa.

"Faida ya miradi ya maendeleo haiwezi kuonekana leo,lakini baada ya miaka kadhaa tutaona faida ya miradi hiyo,ijapokuwa miradi ya barabara tayari ishaanza kuleta faida na wananchi kuweza kufaidika.Katika mkutano huo,Dk.Michael aliupongeza  uongozi wa TPA kwa ufanyaji wake wa kazi kwa kuwa imekuwa ndio chanzo kikuu cha kuongeza mapato nchini.

Amesema shehena ndio kigezo kikuu cha uendelezaji wa Bandari ya Tanzania ambapo hivi sasa imeongezeka kutoka milioni 14hadi milioni 15.Dk Michael alilitaka Baraza hilo kushirikuana na uongozi wa TPA ili kuweza kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Baraza hilo .Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema,TPA inaendelea kujiwekea malengo ambayo yatakuwa endelevu katika kulisaidia taifa na kukuza uchumi wake.Hata hivo Mhandisi Kakoko amesema dhumuni lao kubwa ni kuongeza shehena nyingi zaidi ili kuweza kuongeza mapato kwa taifa.

,,Uboreshaji wa bandari zetu nchini zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza shehena nyingi zaidi kutoka katika nchi mbalimbali kutokana na kupakana na nchi nyingi ambazo zinategemea bandari zetu"amesema Mhandisi Kakoko.

"Kila nchi inayopakana na bandari zetu za hapa nchini tutafanya nao mazungumzo ili mizigo yao wawe wanaipitisha katika bandari hizo na hilo linawezekana kutokana na mikakati waliojiwekea.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko akitoa utendaji wa mamlaka hiyo katika Mkutano wa 25 wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo uliofanyika Mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
 Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari(TPA) Abraham Lukumay akitoa maazimio ya baraza hilo katika mkutano wa 25 uliofanyika mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt Francis Michael akifungua mkutano wa 25 wa baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari uliofanyika Mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
 Mgeni rasmi katika picha pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi Makao Mkuu
 Mgeni Rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi la TPA katika Mkutano wa 25 uliofanyika Mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
 Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi la TPA wakisikiliza taarifa mbalimbali za baraza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...