Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MKE waliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART) Robert Kisena (46), Florencia Mashauri amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashitaka sita likiwemo shtaka la kuuza mafuta bila kibali na kusababisha hasara ya Sh bilioni 2.4.

Florence ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Zenon, na mkazi wa mtaa wa Isevya Upanga, amefikishwa mahakamani hapo April  10, 2019 na kusomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi, Augustino Rwizile.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali, Ester Martin akisaidiana na Fatuma Waziri, amedai, kati ya Januari Mosi, 2011 na Mei 31,2018 katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa  Florence akiwa na watu ambao hawapo mahakamani, waliratibu genge la uhalifu.
Imeendelea kudaiwa kuwa, kati ya Januari Mosi, 2015 na Desemba 31, 2017 huko katika maeneo ya Jangwani wilayani Ilala mshtakiwa akiwa Mkurugenzi wa Zenon Oil & Gas Limited, alijenga Kituo cha mafuta cha Petroli kilichopo yadi ya Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Imedaiwa, mshitakiwa huyo ambaye anajulikana pia kwa jina la Florencia Membe, akiwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo, alianzisha biashara ya kuuza mafuta katika eneo lisiloruhusiwa.

Katika shtaka la nne,  imedaiwa kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 maeneo ya Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDA-PLC), aliiba mafuta ya Sh 1,216,145,375.10 mali ya UDA

Aidha imedaiwa,  kwa lengo la kuhalalisha au kuficha uhalisi alibadili mafuta ya Sh 1,216,145,375.10 kwa kuyauza wakati akijua kwamba mafuta hayo ni zao la uhalifu. Pia mshtakiwa Florence anadaiwa kumiliki Sh bilioni 1.2 huku akijua kwamba fedha hizo ni zao la kosa la wizi.

Katika mashitaka ya kuisababishia serikali hasara inadaiwa kuwa kati ya tarehe hizo, Florence  aliisababishia UDART hasara ya Sh 2,414,326,260.

Hata hivyo, mshitakiwa hukuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi  ambazo kwa kawaida husikilizwa Mahakama Kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP.

Kwa Mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.  

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 23, kesi hiyo itakapokuja tena mahakamani hapo kwa kutajwa, mshitakiwa amerudishwa rumande

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...