Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shanna alipotembelea eneo la oldonyosambu ajali ilipotokea jana na kusababisha vifo vya watu wawili.
Kamanda wa wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shanna akitolea ufafanuzi ajali iliyotokea jana eneo la Oldonyosambo barabara ya Arusha Namanga.,Kulia kwakwe ni mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani hapa Joseph Bukombe
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akipokea maelezo kitoka kwa Dkt. Wa Halmashauri ya Arusha Petro Mboya katika hospital ya Seliani
Mkuu wa wilaya ya Arumeru jerry Muro akimjulia hali mmoja wa majeruhi aliyelazwa katika hospitali ya Seliani Ngaramtoni.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya Arusha Dkt Petro Mboya akifafanua jambo kwa mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro.


Na. Vero Ignatus, Arusha

Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limetoa onyo kali kwa madereva ambao wanendesha magari bila kufuata sheria usalama barabarani na kusababisha ajali katika kupoteza maisha ya watu sababu ya uzembe.

Onyo hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Arusha kutokana na ajali iliyotokea jana eneo la Oldonyosambu na kusababisha vifo vya watu 2 na wengine 5 kujeruhiwa vibaya, amesema kwa dereva atakayekutwa na kosa la uzembe sheria itafuata mkondo wake.

Vilevile RPC Shanna ametoa onyo mitandao ya jamii ambayo inatoa taarifa ambazo siyo sahihi hazijathibitishwa, amesema mitandao mingi hapo jana ilieneza uvumi kwamba watu waliofariki ni 8 wakati siyo kweli na ikaleta taharuki katika jamii.

Amewataja majina kuwa ni bwana Robby Alan (kenya) Rajab Essa (mmakoe) (31)mkazi wa Arusha, Robby Mkurya (kenya) Anold Twahir (mshirazi) mkazi wa Arusha Shadrack Anold (13)ni mwanafunzi mkazi wa Arusha, Stellah Mathon Mngai(kenya ) (21)Bosco Mshanga mkazi wa Arusha wote hawa walikuwa abiria ndani ya magari hayo na wawili kati yao hali zao ni mbaya.

RPC amesema mbali na tukio hilo lililoleta majonzi, mkoa wa Arusha upo swari hakuna matukio mengine katika msimu huu wa sikukuu wala uhalifu kwani jeshi la polisi lilijipanga vilivyo na wananchi walionyesha ushirikiano mkubwa.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro amekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ajali ya Oldonyosambu inayodaiwa kuwa katika ajali hiyo watu nane Walifariki dunia kitu ambacho siyo kweli katika ajali hiyo watu wawili ndio Walifariki dunia.

Muro Ameyasema hayo mara baada ya kuwatembelea Majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika Hospitali ya Selian Lutheran Ngaramtoni ambapo ilitokea katika eneo la Oldonyosambu na kuwataka wananchi kuacha kukurupuka na kuandika ovyo katika mitandao ya kijamii vinavyozua taaruki pindi tatizo linapotokea badala yake wasubiri taarifa kutoka mamlaka husika.

Amewataka wananchi wa Arumeru na mkoa wa Arusha iwapo watataka kufanya matukio yoyote ambayo yatakuwa na kusanyiko lolote linalolenga shughuli pembezoni mwa barabara lazima tukio hilo liripotiwe kwa serikali ili serikali iwaandalie vitu vya Usalama na watu waache kufanya vitu kwa mazoea kwani serikali haiendeshwi kwa mazoea.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa wilaya ya Arumeru Petro Mboya amekiri kupokea miili miwili ya watu waliofariki hapo jana,majeruhi ambao wanaendelea kutibiwa ambapo wawili wameumia vichwani, mmoja uti wa mgongo na wengine wapo ICU ambapo mmoja wamemuhamisha kwaajili ya kufanyiwa vipimo zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...