Na Agness Francis, blogu ya Jamii. 

ZIMEBAKI siku 4 wawakilishi wa Tanzania   klabu bingwa barani Afrika Simba SC kuwavaa TP Mazembe ya nchini Congo katika mchezo wa robo fainali. 

Mchezo huo utakaoanza kutimua vumbi majira ya saa kumi jioni Aprili 6 mwaka huu katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salam kwa viingilio vya 4000 mzunguko, VIP B 10000, VIP A 20000, huku tiketi za platinum zikiuzwa kwa 100,000, na mchezo wa marudiano kati ya timu hizo utafanyika April 12 2019 mjini  Lubumbashi huko nchini Congo.

Msemaji wa   Simba SC Haji Manara akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kuelekea mchezo huo
 kauli mbiu yao ya Yes we can ndio itakayotumika tena  dhidi ya mchezo huo, ambapo pia ilitumika kwenye hatua ya makundi dhidi ya JS Saoura na Allyahal ambapo walifanikiwa kupata matokeo mazuri wakiwa katika uwanja wa nyumbani. 

"Tunakwenda na Slogan ile ile ya Yes We Can, kwa sababu imelipa na inatuweka salama zaidi huku tukicheza bila wasi wasi Tutawakabili Mazembe huku tukiujua ubora wao lakini Simba ishazoea kuishangaza Afrika na Dunia kwa ujumla na tutafanya hivyo Jumamosi na tutaendelea na kauli mbiu hiyo tutakapokwenda Lubumbashi Congo katika mchezo wa marudiano Insha'Allah" Haji S Manara Afisa habari Simba Sc.

Hata  hivyo Msemaji huyo amekanusha uvumi unaozagaa kuhusu mgomo wa Nyota wao  tegemezi Emmanuel Okwi raia wa Uganda pamoja na Cloutous  Chama kutoka nchini. 

"Sio kweli kuhusu taarifa zinazozagaa kuhusu kugoma kwa wachezaji wetu hao, walipata ruhusa ya mwalimu na sasa wamesharejea kambini kuendelea na mazoezi pamoja na wenzao" amesema Manara. 

Manara amemalizia kwa kusema kuwa "hakuna  mchezaji kutoka Afrika Mashariki anayeweza kugoma kuchezea Simba, tumepoke maombi mengi kutoka kwa wachezaji wa ndani na nje ya nchi kwa barua ili tuwasajili na wengine wanaotoka klabu kubwa tu hapa nchini kila mtu anataka kuchezea Simba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...